Breaking News

Your Ad Spot

May 27, 2011

MKE WA WAZIRI MKUU WA INDIA AIMWAGIA WAMA SH. MILIONI15

Mama Salma Kikwete akikabidhiwa hundi ya Sh. milioni 15 na MamaKaur










































Ziara ya Waziri Mkuu wa India  Dk. Manmohan Sigh imeshusha neema kwa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) baada ya mkewe, Mama Gursharan Kaur kuipa WAMA msaada wa sh.  milioni 15 kwa ajili shughuli mbalimbali za kuwasaidia watanzania zinazofanywa na taasisi hiyo.

Mama Kauri  ameukabidhi msaada huo leo kwa Mwenyekiti wa  WAMA Mama Salma Kikwete, alipotembelea Ofisi za Taasisi hiyo, mjini Dar es Salaam.


Akikabidhi  hundi ya fedha hizo, Mama Kaur alisema kuwa ameguswa na kazi zinazofanywa na WAMA za kuisaidia jamii ya kitanzania, hivyo msaada huo utasaidia kutekeleza majukumu mbalimbali wanayoyafanya.

Kwa upande wake Mama Kikwete alishukuru kwa msaada huo na kusema kuwa fedha hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua matatizo yanayoikabili jamii ya kitanzania.

Alisema kuwa taasisi ya WAMA imekuwa ikipokea misaada mbalimbali kutoka kwa wadau wa maendeleo wa ndani na wa nje ya nchi hivyo aliwaomba wananchi wenye moyo wa kusaidia wasisite kufanya hivyo bila ya kuangalia kama msaada watakaoutoa ni mdogo au mkubwa.

Mama Kikwete alisema kuwa Taasisi ya WAMA imekuwa ikifanya kazi mbalimbali za kuhakikisha kuwa inawasaidia wanawake kuinua maisha yao, kuisaidia jamii ya watanzania kuwa na afya bora, kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI kwa vijana na kada tofauti, kushughulikia uzazi salama  na kuwawezesha watoto wa kike ambao ni yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu kupata elimu.

Mama Kaur ameambatana na mumewe waziri Mkuu wa India Dr. Manmohan Singh aliyeko nchini katika ziara ya kikazi ya siku tatu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages