Breaking News

Your Ad Spot

May 24, 2011

NAPE ATEMBELEA UDOM LEO, AAGIZA MAJENGO YENYE NYUFA YASHUGHULIKIWE HARAKA

CCM imewaagiza viongozi wanaohusika kwenda kukagua majengo ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) ili kulipatia ufumbuzi wa haraka tatizo la nyufa zilizoanza kuitokeza kwenye baadhi ya majengo.

Chama kimewaagiza pia viongozi hao kukagua hali ya miundombinu ya majitaka katika maadhi ma maeneo chuoni hapo ili ifanyiwe marekebisho kwa kuwa inatuamisha maji kutoka katika majengo na kusababisha adha ya harufu mbaya kwa wanafunzi, walimu na wafanyakazima,m wengine chuoni hapo.

Maagizo hayo yalitolewa leo, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, baada ya kutembelea chuo hicho na kagua baadhi ya majengo ambapo alishuhudia baadhi ya majengo yakiwa na nyufa.

Majengo yaliyoonyesha kuwa na nyufa ni katiba mabweni ya wanafuzi wa Shule ya Sayansi na Jamii yaliyoko Block 2 na 3 ambapo alionyeshwa na wanafunzi wanaoishi katika mabweni hayo.

"Kujengwa kwa chuo hiki ni uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, hivyo ni lazima kuuenzi uamuzi huu kwa kuhakikisha mazingira na majengo yake yanakuwa katika hali bora", alisema Nape.

Nape alionyesha kushangazwa kwake kuona majengo ambayo hayajatimiza miaka mitano tangu kujengwa kwake, kuanza kupata nyufa jambo ambalo alisema ni hatari kwa usalama wa wanafunzi wanaoishi katika majengo hayo.

Mapema akizungumza na Nape, ofisini kwake, Makamu Mkuu wa UDOM Profesa, Idrisa Kikula alisema, sasa chuo hicho kina wanafunzi 20,000 ambao kati yao asilimia 50 wanalipiwa gharama zao zote za masomo na Bodi ya Mikopo.

Profesa Kikula alisema, wakati chuo hicho kina wanafunzi pia kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Msumbiji, Walimu wapo kutoka nchi za Russia, India, Kenya, Nigeria,Korea, Japan, Poland na Sweden.

Alisema, moja ya changamoto zinazokabili chuo hicho ni uhaba wa walimu kwa kuwa waliokuwepo zamani wengi ni wazee au wanaugua magonjwa mbalimbali yanayoambatana na utu uzima.

Profesa Kikula alisema, changamoto hiyo ya uhaba wa walimu imesababisha chuo hicho kuendelea kupokea wanafunzi wasiozidi 20,000 tu, wakati kina uwezo wa kuwa na wanafunzi hadi 35,000.


Alisema, katika kukabiliana na changamoto hiyo, chuo kimeajiri vijana zaidi ya 300, lakini ili  walimu zaidi ya 200 kati ya hao 300 wapo masomoni ndabi na nje ya nchi kwa lengo la kuwa na wahadhiri wasaidizi wengi.

Ziara ya Nape mjini Dodoma amabayo ilimalizika jana, ilianza Jumatatu wiki hii, ambapo alihudhguria sherehe za kuagwa wanafunzi wa UDOM wa mwaka wa tatu ambao ni makada wa CCM.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages