Breaking News

Your Ad Spot

Jun 14, 2011

JOSE MARA ATANGAZA KUWAKACHA RASMI WAZEE WA NGWASUMA

Aliyekuwa mwanamuziki mwenye sauti mwanana na yenye mvuto wa kipekee  wa bendi ya FM Academia aka Wazee wa Ngwasuma, Jose Mara amejiondoa rasmi katika bendi hiyo.

Akikaririwa na Blogu ya Dina Ismail,  Jose Mara amesema amejitoa FM  Academia ili kuweza kuitumikia vema bendi yake ya Mapacha Watatu akiwa  na  wachapakazi wenzake kina Khalid Chokoraa na Kalala Junior.

Bendi ya Mapacha Watatu iliyoanza kama bendi ya 'zing zong' imejipatia umaarufu kwa muda mfupi kutokana na kupiga muziki wenye midundo mchanganyiko na hivyo kujizolea mashabiki kibao.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages