Breaking News

Your Ad Spot

Jun 1, 2011

NAPE, MWIGULU WAITEKA SUMBAWANGA

    NA MWANDISHI WETU, SUMBAWANGA

KATIBU wa NEC ya CCM, Itikati na Uenezi Nape Nnayue na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Nchemba Mwigulu, waliuteka mji wa Sumbawanga, baada ya mamia ya wananchi kufurika kwenye mkutano wa hadhara katika uliofanyika katika Uwanja wa Mndela mjini hapa.
      Kimbunga cha mkutano huo, kiliwazoa wananchi 51 waliokuwa wanachama wa CHADEMA ambao kutokana na furaha yao, waliamua kukabidhi kadi zao kwa Nape na kutangaza kujiunga na CCM. "Tunaachana na ujinga wao", alisema mmoja wa wananchi hao, Geofrey Mwanakatwe wakati akikabidhi kadi yake ya Chadema kwa Nape.
      Hadi saa tisa alasiri uwanja huo ukiwa umefurika wananchi, msafara wa Nape na Mwigulu, uliigia na kusababisha uwanja huo kulipuka kwa nderemo na vifijo kuwashangilia.
        Mwigulu ndiye alikuwa wa kwanza kuhutubia kwenye mkutano huo nchi baada ya kukaribishwa jukwaani na Nape.
       Akionyesha umahiri wake katika masuala ya uchumi, Mwigulu alisema, wanasiasa wa vyama vya upinzani kama CHADEMA ambao wamekuwa wakihamasisha wananchi kukataa kuchangia miradi ya maendeleo ni wanasiasa hao ni tatizo kwa taifa.
       Mwinguli alisema, anazo taarifa kwamba viongozi hao wamekuwa waki wakiwaambia wananchi kwamba hawana sababu ya kuchangia kwenye miradi hata inayoanzishwa katika maeneo yao kwa kuwadanganya kuwa jukumu lote ni la serikali.
        Aliwataka wananchi kutowasikiliza wnasiasa hao akisema wanachofanya wanaviza akili za wananchi, kwa kuwa hakuna nchi inayoweza kupata maendeleo bila maendeleo hayo kuhangiwa na wananchi.
       "Wananchi kataeni mawazo ya aina hii, kwanza ukiona mtu anakukataza kuchangia maendeleo ujue huyo anajihami usimuombe kukuchangia na wewe, achaneni nao kabisa", alisema Mugulu.
       Baada ya hotuba ya Mwigulu, kipaza sauti kilihamaia kwa Nape, ambaye alitoa hotuba yenye kuchoma hisia za watu na kusababisha baadhi ya wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo hasa vijana, kujipiga vifua mfano wa muumini aliyeingiwa na roho mtakatifu kwenye mkutano wa mahubiri ya kidini.
        Mbali na uwezo wake wa kugusa hisia za watu wakati akihutubia, maneno yake yaliwagusa wananchi, hasa pale alipofafanua kwa kina na kwa umahiri mkubwa maana ya CCM kijivua gamba na maana ya kujivua gamba kwenyewe ni nini.
         Alisema, kujivua gamba kwa CCM hakumaamishi kwamba Chama kimebadili tabia yake iliyoasisiwa nayo na viongozi walioianzisha akiwemo Baba wa Taiafa, Hayati Mwalimu Nyerere, ila imebaki pale pale katika msingi yake na wala haikubaki na uzembe na ufisadi ulioonyeshwa na badhi ya viongozi wake kabla ya mabadiliko hayo.
        "Tulichofanya ni kama afanyavyo nyoka. Baada ya kupatwa na dhoruba kwa muda mrefu katika maisha yake huishiwa uwezo wa mambo mengi, ikiwemo kukimbia, kunusa na hata kupungua ukali wa sumu yake na kwa uwezo wa Mungu hujibua gaamba na kubaki na ngozi mpya ambayo sasa humfanya kuwa na uwezo wake wa awali au uwezo huo kuongezeka", alisema Nape na kuongeza:

      "Hivyo ndivyo CCM nayo ilivyofanya. Baada ya kuongoza kwa muda mrefu tukaona Chama kinaanza kupotoka katika misingi yake. Tukasema hizi ni dalili za kuchakaa gamba, tulivue, tukakubaliana kujivua na kufanya uamuzi mgumu ambao chama kingine kisicho na misingi bora hakiwezi".
        Alisema, kutokana na hatua hiyo sasa CCM imepata ngozi mpya, na tabia zake ambazo ni itikadi na malengo yake ya kuanzishwa sasa yameongezeka ili kuleta upendo ulipokuwa umeanza kujaa kupotea,kuleta amani pale ilipokuwa imeanza kutetereka, kuleta matumaini pale yalipokuwa yameanza na kuongeza uwezo wa sumu ya kuitemea serikali katika kuisimamia kutekeleza ilani ya Chama.
       Nape aliwataka wananchi hasa vijana waliokuwa wameanza kukata tamaa, kurejesha imani zao kwa CCM, kwa kuwa ndicho chama chenye uhakika wa kusimamia maendeleo na amani na utulivu.
        Alikemea viongozi wa CHADEMA ambao wamekuwa wakisema kwamba nchi haitatawalika, akisema kwamba viongozi hao wanatamba kusema maneno hayo  kwa sababu hawajui uchungu wa nchi ilivyohangaika kujenga mshikamano wa kitaifa na amani na utulivu uliopo.
       Nape alirejea kauli yake kwamba, kauli hiyo ni ndoto za mchana na kuwatukana Watanzania ambao wanafahamu kuwa wameipa CCM ridhaa ya kuongoza ili nchi itawalike.
Katika ziara hiyo, Wajumbe hao wa sektretarieti wanatarajia kufanya mikutano kadhaa ya hadhara mkoani Rukwa katika maeneo ya Namanyere, Kabwe, Maji moto, Usevya, Kakese na Mpanda mjini.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages