Breaking News

Your Ad Spot

Jul 13, 2011

WAHARIRI 80 KUTOKA BARA NA VISIWANI KUNOLEWA ARUSHA

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwa kushirikiana na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), wameandaa mkutano wa kitaaluma wa wahariri utakaofanyika Arusha kuanzia Alhamisi, Julai 14 hadi Jumamosi, Julai 17, 2011.

Mkutano huo utawashirikisha wahariri wapatao 80 kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ambapo mada kuu ni “Responsible Journalism” kwa tafsiri isiyo rasmi ni Uandishi wa Habari unaozingatia Wajibu’.

Miongoni mwa mada zitakazowasilishwa na kujadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na hali ya utendaji wa vyombo vya habari, maadili ya waandishi wa habari ndani na nje ya vyumba vya habari, athari za uandishi wa habari unaoegemea upande mmoja, makosa katika utangazaji na uandishi wa habari na wajibu katika habari za michezo.

Mbali na mada hizo, wahariri watapata fursa ya kutembelea kiwanda kipya cha kuzalisha bia kilichopo mjini Moshi. Pia kutakuwa na mchezo wa mpira wa miguu kati ya jukwaa la wahariri na timu ya wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti katika uwanja wa TPC siku ya Jumamosi tarehe 16Julai.

Mbali na hayo, wahariri watashiriki katika tamasha kubwa la muziki la Serengeti Fiesta litakalofanyika Jumamosi katika uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungenzi wa SBL, Jaji Mark Bomani atatoa Mada ya Ufunguzi kwa wahariri Alhamisi jioni na wahariri wataendelea na mkutano wao wa ndani Ijumaa Julai 15,2011. 

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda akiteta jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (SBL) Teddy Mapunda, viongozi wa jukwaa hilo walipokutana na waandishi wa habari leo kwenye hoteli ya Movenpick Dar es Salaam, kuzungumzia mkutano huo wa wahariri 
Katibu wa Jukwaa la Wahariri, Neville Meena akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kutangaza kufanyika kwa mkutano wa siku tatu wa wahariri wa habari kujinoa, utakaofanyika mjini Arusha wiki hii. Wengine ni  Mjumbe wa Bodi wa Jukwaa la wahariri, Godfrey Chongolo (kushoto), Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Absalom Kibanda , Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni ya Bia ya serengeti (SBL) Teddy Mapunda, Mjumbe wa Bodi ya Jukwaa la wahariri, Masoud Sanani na Meneja Mawasiliano ya Ndani wa SBL, Imani Lwinga.  
Teddy akimkabidhi vifaa vya michezo kwa ajili ya mechi maalum kati ya Jukwaa la Wahariri na SBL baada ya mkutano huo mjini Arusha. 
Teddy akimuonyesha Sanani jezi itakayotumiwa na timu ya SBL. Mkutnao huo wa leo umefanyika katika hoteli ya Movenpick Dar es Salaam

Badhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo Movenpick

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages