Breaking News

Your Ad Spot

Aug 23, 2011

MBUNGE SILIMA AFARIKI KUFUATIA AJALI YA GARI ILIYOTANGULIA KUMUUA MKEWE

Silima
Mbunge Mussa Hamisi Silima, aliyejeruhiwa baada ya kupata ajali jana mjini hapa,
amefariki dunia.
      Silima alifariki dunia leo saa tano asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam ambako alihamishiwa na kulazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu
zaidi.
        Taarifa za kifo cha Silima zilitangazwa jana saa 5.50 asubuhi na Spika wa Bunge, Anne Makinda wakati wabunge wakiendelea kuchangia makadirio ya mapato na
matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2011/2012.
       "Waheshimiwa wabunge, kama mtakumbuka jana niliwatangazia kwamba,
mheshimiwa Mussa Hamisi Silima, alipata ajali mbaya eneo la Nzuguni, ambapo
mke wake, Mwanaheri Twalib alifariki dunia hapo hapo.
    "Aidha niliwaarifu kuwa, mheshimiwa Silima na dereva wake walipata majeraha makubwa na wamepelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi. Leo asubuhi kabla ya maswali,nimetoa taarifa kwenu kwamba nimeongea na mheshimiwa Silima akiwa anaendelea kupata matibabu. Ni kweli nimeongea naye.
          "Kwa masikitiko makubwa, nawatangazieni kuwa, nimepokea taarifa kutoka kwa katibu mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii kwamba, mheshimiwa Mussa Hamisi Silima amefariki dunia muda mfupi tu uliopita.
        "Kwa mujibu wa kanuni ya 149 ya kanuni za bunge, toleo la mwaka 2007, ninaahirisha shughuli za bunge mpaka kesho saa tatu asubuhi," alisema.
         Kufuatia msiba huo, Spika Anne aliwataka wabunge wasimame kwa dakika moja kwa heshima ya mbunge huyo.
Spika alisema kwa kipindi cha siku tatu, familia ya Silima imekumbwa na matatizo makubwa, kufuatia kutanguliwa na msiba wa kaka wa mkewe kabla ya mkewe naye kufariki dunia.
  Katika ajali iliyotokea jana eneo la Nzuguni, mke wa mbunge huyo, Mwanaheri
alikufa papo hapo eneo la ajali wakati dereva wake, Chizali Sembonga, aliyekuwa
akiendesha gari aina ya Toyota Corolla, lenye namba za usajili T 509 AGC
alijeruhuwa.
Silima na mkewe walipatwa na ajali hiyo walipokuwa wakirejea Dodoma. Mbunge
huyo alikuwa amekwenda Zanzibar kuhudhuria maziko ya kaka wa mkewe,
Mwanaheri.
Mbunge huyo na dereva wake walisafirishwa kwa ndege juzi kwenda Dar es
Salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Mwili wa Mwanaheri ulizikwa juzi alasiri

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages