Breaking News

Your Ad Spot

Sep 30, 2011

MKAPA ATINGA IGUNGA JIONI HII, KUFUNGA KAMPENI ZA CCM KESHO

                                                                                                                 
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akisalimiana
na wananchi baada ya kuwasili kwenye hoteli aliyofikia mjini Igunga
 leo jioni

 Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amewasili jioni hii mjini Igunga.

Kufuatia kuwasili kwake, kesho atafunga kampeni za CCM katika mkutano unaotarajiwa kuwa mkubwa, kwenye Uwanja wa Sokoni, Kata ya Nkiga.

Mkapa aliwasili kwa msafara wa magari na kulakiwa naviongozi mbalimbali wa CCM mkoa wa Tabora, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama.
Baada ya kupokewa na viongozi hap msafara wa Mkapa ukipambwa na waendesha pikipiki, baiskeli, bajaji ulikwenda hadi katika hoteli maarufu ya mjini Igunga, The Peak Hotel ambako alipata mapumziko na baadaye kuwa na mazungumzo na viongozi wa Chama wa mkoa na wilaya ya Igunga.

Mkapa kufunga kampeni hizo, kutamfanya kuweka historia ya aina yake katika medani ya Siasa kwa kuwa yeye ndiye alifungua mkutano wa kampeni za CCM mjini hapa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.

Mbali na Mkapa kufunga kampeni katika mkutano huo, CCM pia itakuwa na mikutano mingine ya kampeni za mwisho ambayo kwa mujibu wa ratiba itafanyika Mwanzugi, Choma, Ziba, Igurubi, Uswaya na Nsimbo.

Uchaguzi mdogo jimboni hapa utafanyika Jumapili hii, baada ya kampeni za vyama vinane vinavyoshiriki uchaguzi huo ambao unafanyika kufuatia kujiuzulu aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Rostam Aziz.

1 comment:

  1. Wewe na viongozi wako wote hao ni wizi tu. Kuanzia Mkapa, Kikwete wote wasanii, tunataka mabadiliko, yanawezekana tu. Zambia, Kenya, na nchi nyingine wameweza.

    Mdau
    Sweden

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages