Breaking News

Your Ad Spot

Nov 16, 2011

TIMU YA TAIFA YA POOL TABLE YAENDA MALAWI KWENYE MASHINDANO YA ALL AFRICA CUP

Timu hiyo ikikabidhiwa bendera ya taifa leo jijini Dar

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imetangaza rasmi kuondoka kwa  timu ya Taifa katika mashindano ya ALL AFRICA CUP 2011-BLANTYRE- MALAWI yanayotarajiwa kuanza tarehe 22.11.2011 hadi 26.11.2011.
 
Akitangaza safri hiyo, Meneja wa bia ya Safari Lager,  Oscar Shelukindo alisema timu hiyo inaondoka leo kufuatia  Bia ya Safari Lager, kukamilisha mahitaji yote muhimu ya Timu ya Taifa kwa ajili ya safari hiyo na kukumbusha kwamba bia hiyo ndiyo mdhamini mkuu wa mchezo wa Pool hapa nchini, na imekuwa ikiidhamini timu ya Taifa ya mchezo wa pool table tangu mwaka 2008 kwenye mashindano ya Africa na Dunia. 

Alisema ikiwa njiani kwenye Blantyre Malawi, timu itapita katika baadhi ya mikoa na kucheza mechi za kirafiki na timu za mikoa hiyo ambayo aliitaja kuwa ni Morogoro, Iringa, Mbeya, Kyela- Mbeya na Kasumulo boarder- Mbeya na kwamba  ni muda mwafaka kwa wananchi kuangalia timu yenu na kuona jinsi ilivyojiandaa.

Naye kocha mkuu wa timu ya taifa, Denis Lungu aliwataja  wachezaji wa timu ya Taifa inayotarajia kuondoka leo.






1
OMARY AKIDA - KINONDONI


2
FELIX ATANAS- DODOMA


3
GODFREY MHANDO- KINONDONI

4
MOHAMED IDDY- KINONDONI


5
CHARLES VENANCE- TEMEKE- CAPTAIN


6
 ANTONY THOMAS- ILALA


7
 SHAMIS NASSORO- ILALA


8
 ABDALLAH HUSEIN- KINONDONI


Akiongelea kuhusu mashindano hayo, Katibu wa chama cha Pool Taifa Bw. Amos Kafwinga alisema, ”Katika mashindano ya mwaka huu ya ALL AFRICA CUP yanatajiwa kushirikisha nchi 14 wanachama wa ALL AFRICA POOL ASSOCIATION (AAPA) na nchi hizo ni Africa kusini, Tanzania, Malawi, Zimbabwe, Cameroon, Zambia, Uganda, Swazland, Reunion FFB, Reunion Arabas, Nigeria , Msumbiji, Morocco na Lesotho.

Akitoa salam za shukrani kwa Safari Lager kwa niaba ya Chama cha Mchezo wa Pool Tanzania (TAPA), Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Isaac Togocho alisema “ Mchezo wa pool table sasa umekuwa si mchezo tena wa kupoteza muda bali ni mchezo kama michezo mingine na unaelekea kuwa ajira rasmi kwa vijana wa Tanzania. Ningependa kutoka shukrani za kipekee kwa Safari Lager na TBL kwa ujumla kwa kuweza kuiweka Tanzania katika ramani ya michezo kimataifa kupitia SAFARI LAGER BEER ni fahari kubwa kwa mchezo wa pool table Tanzania. TAPA inaahidi kuendeleza ushirikiano huu mzuri na mdhamini kwa kusimamia na kuendeleza mchezo huu wa Pool hapa nchini.”

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages