Breaking News

Your Ad Spot

Jan 2, 2012

MWENYEKITI WA TAIAFA JUMUIA YA WAZAZI CCM, MZEE MHINA AFARIKI

Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuia ya Wazazi CCM, Athumani Mhina amefariki dunia.
     Taarifa za awali zilizopatikana kutoka vyanzo vya uhakika, zimesema Mzee mhina amefariki usiku wa kuamkia leo wakati akipelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupatiwa matibabu baada ya kuzidiwa.
      Kwa mujibu wahabari hizo mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Jeshi Lugalo, na unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda kijiji cha Mnyuzi wilayani Korogwe mkoani Tanga, kwa mazishi.
       Mnyuzi ni kijiji kilichopo jirani na kijiji cha Mahezangulu cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Mzee Yusuf Makamba.
       Kwa mujibu wa taarifa, kabla ya kusafirishwa, mwili  utaagwa nyumbani kwa marehemu, Kijiji cha Mivumoni, Madale, Kata ya mpya ya Wazo, wilaya ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages