Breaking News

Your Ad Spot

Jan 28, 2012

RAIS KIKWETE AKUTANA NA BOSI WA Vodafone MJINI DAVOS


Rais Kikwete na Bosi wa Vodafone mjini Davos
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo mafupi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vodafone Bw. Vittorio Colao mjini Davos, Uswisi.

Vodafone ndio wanahisa wakuu wa kampuni ya Vodacom Tanzania.

Bw Colao ambae anahudhuria mkutano wa Uchumi wa Ulimwengu – WEF mjini Davos kama ilivyo kwa Rais Kikwete walipata nafasi ya kukutana na kufanya mazungumzo hayo katika hoteli ya Sheraton Waldhuus.

Mazungumzo hayo yaligusia mahusiano ya Vodafone na seriklai ya Tanzania na watu wake hususan katika uwekezaji katika jamii kusaidia kukuza,kuimarisha na kuboresha huduma za kijamii nchini ikiwa ni utekelezaji wa azma na malengo makuu ya Vodafone ya kuchangia kubadili maisha ya watanzania.

Vodafone kupitia Vodacom Tanzania imekuwa ikiwekeza kiasi kikubwa cha fedha kusaidia na kuunga mkono miradi mbalimbali ya kijamii nchini ikiwemo maeneo makuu matano ya Elimu, Afya, Kuinua vipato vya wanawake, Mazingira na Michezo ili kuunga mkono juhudi za serikali zinazolenga  kuwaletea wananchi maendeleo

Katika mazungumzo hayo mafupi Bw. Colao alimuhakikishia Rais Kikwete kwamba Vodafone itaendelea kuwekeza katika maendeleo ya jamii Tanzania hususan katika maeneo ya afya na elimu ambayo yanauhusiano wa moja kwa moja na wa karibu katika kuiwezesha jamii kuondokana na changamoto ambazo zinaweza kuathiri maendeleo ya watu na hivyo kushindwa au kupunguza kasi ya kubadili maisha yao.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages