Breaking News

Your Ad Spot

Feb 13, 2012

KIKAO CHA NEC CCM KILIVYOMALIZIKA KWA ANAMI DODOMA

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akiwasili ukumbini kuendesha kikao cha NEC mjini Dodoma jana. Kushoto  ni Mwenyekiti mstaafu wa CCM Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Wanzibar  Dk. Ali Mohamed Sheni na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Amani Abeid  Karume. Kulia Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akisisitiza jambo kwenye kikao hicho. Kushoto ni Rais wa Zanzibar Dk. Sheni na Makamu Mkt (Zanzibar) Amani  Abeid Karume
 Kicheko: Rais Kikwete, Mukama na Msekwa wakicheka baada ya kufurahishwa na hoja za wajumbe wakati wa mjadala wa marekebisho ya Katiba ya CCM
 Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Ali Hassan Mwinyi akifurahia jambo wakati wa kikao cha NEC mjini Dodoma juzi.
 Rais Kikwete akijenga hoja katika mkutano huo
 Wajumbe wa NEC kutoka Tanzania Bara wakinyoosha mikono kuunga mkono marekebisho ya katiba ya CCM ambayo yalipitishwa na kikao hicho
 Rais Kikwete, Mukana na Msekwa wakiongoza kunyoosha mikono kuunga hoja hiyo
 Wajumbe wa NEC Zanzibar wakinyoosha mikono kuunga mkono kupitishwa kwa marekebisho ya Katiba ya CCM
Baada ya mabadiliko ya Katiba na baadhi ya ajenda kupitishwa, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akazungumza na waandishi wa habari kuhusu yaliyojiri kikaoni

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages