Breaking News

Your Ad Spot

Feb 18, 2012

RAIS KIKWETE AONGOZA MATEMBEZI YA KUPAMBANA 'FESTULA' YALIYOANDALIWA NA VODACOM NA CCBRT

Rais Dk.Jakaya Kikwete akishiriki mazoezi kabla ya kuongoza matembezi ya kampeni ya Moyo Challenge iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania na CCBRT kuhamasisha uchangiaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya CCBR kwa ajili ya kinamama wenye matatizo ya fistula waweze kupata huduma bure hapa nchini, Kushoto ni Rais wa Bodi ya Wakurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Dk. Wilbroad Slaa, na Watatu ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hajj Mponda na wengine ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT Erwin Elemans na Ofisa Mkuu wa masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba. Kuchangia kwa M-PESA unatuma  kwenda namba 200500, na kwa njia ya SMS tuma neno Moyo kwenda namba 15599.
 Jk akiwa kwenye mazoezi kabla ya matembezi hayo
 Rais Dk.Jakaya Kikwete akiongoza matembezi 
 Rais, Dr.Jakaya Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo. Aliyemshikia utepe huo ni Rais wa Bodi ya Wakurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Dk Wilbroad Slaa
  Rais Dk.Kikwete akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza, (kulia)wakati akimweleza jambo kuhusu kampeni hiyo. Wa pili kulia ni Rais wa Bodi ya Wakurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Dk . Wilbroad Slaa na kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Haji Mponda  
RAIS wa Bodi ya Wakurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Dk Wilbroad Slaa akisisitiza jambo kwa Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba (kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT Erwin Telemans katikati,wakati wa matembezi  hayo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages