Breaking News

Your Ad Spot

Mar 17, 2012

LEMA AKIRI KUMHUSISHA DK. BATILDA NA KASHFA YA RICHMOND

MBUNGE wa jimbo la Arusha mjini Godbles Lema amekiri kumuhusisha aliyekua mgombea ubunge wa jimbo la Arusha mjini kwa tiketi ya CCM Dk.Batilda Burian na kashfa ya Richmond.

Habari kutoka Arusha ambako kesi ya madai ya kutaka ushindi wa ubunge wa Lema (pichani) ubatilishwe inaunguruma, zimesema, Lema alimhusisha Dk. Batilda na kashfa hiyo kwa kutamka katika baadhi ya mikutano yake ya kampeni kuwa Dk.Batilda alimwandikia barua mbunge wa jimbo la Same Mashariki(CCM)Anne Kilango Malecela kumuhoji kwanini alizungumzia masuala ya Richmond Bungeni na kumuonya asirudie kulizungumzia kwakua jambo hilo lilikua linamuhusu.

Lema alikiri kutamka hayo kwa madai kuwa siyo mambo yaliyokatazwa na kanuni ya sheria ya maadili ya uchaguzi mwaka 2010 kwakua siyo matusi, kashfa au udhalilishaji lakini akakiri kuwa kauli hizo zote zililalamikiwa na Dk.Batilda kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Arusha mjini na kutolewa maamuzi mbalimbali.

Lema amekiri hayo leo alipokua akiongozwa na wakili wake Method Kimomogolo mbele ya jaji anayesikiliza kesi hiyo ya kupinga matokeo ya ubunge wake ili kutolea ufafanuzi wa utetezi wake alioutoa mahakamani hapo alipokua akihojiwa na wakili wa upande wa mashitaka Alute Mughwai.

Lema aliulizwa maswali na wakili wake huyo kutokana na kielelezo “C” ambayo ni barua ya Agosti 28 mwaka 2010 kutoka kwa Dk.Batilda kwenda kwa  msimamizi wa uchaguzi jimbo la Arusha akilalamikia kuvunjwa kwa kanuni na sheria za maadili ya uchaguzi ya 2010.

Katika barua hiyo ya malalamiko Dk.Batilda alidai kuwa Lema alizungumza katika moja ya mikutano yake na kuwaeleza kuwa Dk.Batilda aliposikia suala la Richmond linazungumzwa bungeni na mbunge Kilango alimuandikia barua ya kuuliza na kisha kumuonya asirudie tena kulizungumza kwakua linamuhusu.

Kutokana na barua hiyo aliyokua akiisoma Lema mahakamani hapo ambayo alikiri kuipokea aliuliwa na wakili wake kama ni kosa kutamka maneno hayo kulingana na sheria ya uchaguzi ambapo Lema alijibu kuwa si kosa na hata leo ingekuwa ndo kampeni angeendelea kuyatamka hadharani.

Kwa mujibu wa barua hiyo ilidai kuwa Dk.Batilda pia alilalamikia suala za uzushi mwingine uliotolewa na Lema dhidi yake kuwa ni kwamba Dk.Batilda na Rais Kikwete kwa wakati huo walikua wameshasaini mkataba wa kuruhusu ujenzi wa barabara ya lami itakayopita katika mbuga ya wanyama ya Serengeti ambayo ilikua ikipingwa vikali na wanaharakati.

Kutokana na barua hiyo Lema aliulizwa na wakili wake kama kweli alitamka ambapo alijibu kwa madai kuwa haikuwa kashfa kwa mujibu wa kanuni za maadili ya uchaguzi na kwamba kelele zake hizo zimewezesha hadi leo hii barabara hiyo haijajengwa.

Pia Lema alikiri kupokea barua iliyomkuta na tuhuma kutoka halmashauri ya manispaa ya Arusha juu ya kuvunja kanuni na sheria ya maadili ya uchaguzi ambapo ilikua ni majibu ya kielelezo “D” ambapo alipewa adhabu ya karipio,taarifa ambayo haikuja aina ya matusi,kejeli,udhalilishaji aliobainika kuufanya.

Hata hivyo Lema alizua vicheko mahakamani hapo baada ya kuulizwa na wakili wake iwapo alifahamu kama mwakili kutoka katika chama chake kwenda katika kamati ya maadili ya uchaguzi ya jimbo kama alihudhuria kikao hicho kilichomwadhibu au laa.

Kesi hiyo itaendelea Jumatatu kwa shahidi wa pili kwa upande wa mashitaka kusimama kizimbani kuongozwa na wakili Kimomogolo ili kutoa ushahidi wake baada ya Lema kumaliza kutoa ushahidi wake leo.

1 comment:

  1. Drop in on us now to

    obtain more facts and facts

    at all events Visit us

    contemporary to grasp more

    knowledge and facts regarding


    [url=http://www.aktualneinfo.waw.pl/2012/03/13/dieta-z-odzywkami/]odzywki[/url]

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages