Breaking News

Your Ad Spot

Mar 23, 2012

TMK WANAUMEFAMILY KUKAMUA MEDIA DAY

Kundi la muziki wa kizazi kipya la TMK Wanaume Family la jijini Dar es Salaam ni miongozi mwa burudani zitakazokuwepo kwenye bonanza la vyombo vya habari linaloandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).

Bonanza hilo litafanyika  Machi 24 mwaka huu ukumbi wa Msasani Beach Club, Dar es Salaam, huku TASWA ikiamini litakuwa bora na la uhakika.

Licha ya Wanaume Family, burudani  nyingine itakuwa bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, ambapo wadhamini ni Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

Tunataka bonanza la mwaka huu liwe la aina yake kuanzia burudani, michezo na mambo mengine yawe ya aina yake.

Bonanza litaanza saa tatu asubuhi hadi saa mbili usiku, ambapo baadhi ya michezo itakayoshindaniwa ni soka ya ufukweni, netiboli, wavu, mbio za magunia, mbio meta 100, kuruka kichura, kuvuta kamba, kucheza muziki na michezo.

Mgeni rasmi katika bonanza hilo atakuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta.

Lengo la bonanza ni kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine, ili kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja na huwa linafanyika mara moja kwa mwaka, likiandaliwa na TASWA

George John
Mwenyekiti Kamati ya Bonanza
23/03/2012

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages