Breaking News

Your Ad Spot

Apr 25, 2012

HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA YAJIPANGA KUKUSANYA ZAIDI YA SH. BILIONI 56 2012/13


Na Rose Jackson,Arusha
Halmashauri ya Manispaa ya jiji la Arusha imepitisha bajeti ya kukusanya  zaidi ya shilingi  bilioni  56  kwa mwaka wa fedha 2012 -2013.
     Akisoma bajeti hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya arusha Estomih Chang’a alisema kuwa bajeti hiyon itatokana na vyanzo mbalimbali vya mapato vilivyopo ndani ya manispaa hiyo.
    Chang’a alisema kuwa mapato ya vyanzo vya ndani ni sh.8,496,078,520,ruzuku toka serikali kuu sh.25,268,023,468,wafadhili sh.22,190,498,099,pamoja na fidia ya vyanzo vilivyofutwa sh.518,610,000.
     Alitaja vyanzo vingine kuwa ni pamoja na matumizi ya mishahara ambapo ni sh.27,316,260,154,matumizi ya uendeshaji sh.4,017,191,792,na miradi y a sh.25,139,758,141.
      Aidha aliongeza kuwa jambo la muhimu katika bajeti ya halmashauri hiyo ni kuelekeza asilimia hamsini ya fedha katika miradi ya maendeleo inayoendelea ikiwemo madarasa ya ghorofa yanayojengwa katika shule ya sekondari ya Felex Mrema,Themi na Sekondari ya Ngarenaro.
     Pia alisema kuwa bajeti hiyo itaelekezwa katika uendelezaji wa shule mpya ya sekondari Suye ili iweze kutoa elimu ya kidato cha tano na sita sanjari na kuanzisha chuo cha ufundi stadi shuleni hapo.
      Vilevile  halmashauri hiyo itakamilisha miradi ya  visima vya maji  maeneo ya kame kama vile kata ya Terrat,Sokoni One na Mushono ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kukarabati barabara za kata zote ikiwemo madaraja na kalavat.
     “hii bajeti sio kwa ajili ya kuendeleza maendeleo tu bali hata katika huduma za kijamii kama vile kutoa mikopo kwa akina mama na vijana ambapo kupitia mikopo hii itawasaidia kujikwamua kiuchumi"alisema Chang'a.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages