.

MBUNGE APATA AJALI YA GARI

Apr 18, 2012


Abass Mtemvu

Mbunge wa Temeke  Abass Mtevu na dereva wake ambaye jina lake hakutajwa, wamenusurika kifo baada ya kupata ajali ya gari  wakiwa njiani kuja Dar es Salaam.


Akitoa taarifa bungeni mchana huu, Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai amesema baada ya ajali iliyosababishia majeraha kadhaa mwilini, Mtemvu na dereva wake wametibiwa katika hospitali ya Morogoro na kuruhusiwa kuja Dar.


"Wamenusurika ingawa wamepata majera kadhaa mwilini, na hivi ninavyozungumza wapo njiani kwenda Dar es Salaam" alisema Ndugai kuwaambia wabunge. 

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª