Breaking News

Your Ad Spot

Apr 25, 2012

SAFARI LAGER YATANGAZA KUKAMILIKA KWA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI WA “WEZESHWA NA SAFARI LAGER”.



Oscar Shelukindo akizungumza leo
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi kukamilika kwa mafunzo ya wajasiriamali waliopatikana katika shindano la “Wezeshwa na Safari Lager”. 
        Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema mafunzo kwa wajasiriamali wa“Wezeshwa na Safari Lager” yalikamilika rasmi mwishoni mwa wiki katika mikoa ya Dar Es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya.
        Aliwapongeza wajasiriamali wote waliofaulu na kupatiwa mafunzo haya yanayolenga kuwawezeshwa kupanua na kukuza biashara zao. Akielezea mchakato wa kuwapata wajasiriamali hawa Bwana Shelukindo alisema baada ya kutangaza kuanza kwa shindano hili mwishoni mwa mwaka jana, jumla ya fomu za maombi 9,738 zilikusanywa.
        Fomu hizi zilikaguliwa na majaji wenye ujuzi wa mambo ya biashara na wajasiriamali 80 walichaguliwa kuingia katika hatua ya pili. Wajasiriamali waliochaguliwa walitembelewa na wataalamu ili kuthibitisha uwepo wa biashara zao, jumla ya wajasiriamali 54 walifaulu na ndio waliopatiwa mafunzo.
        Wajasiriamali 26 waliondolewa katika hatua hii kutokana na mapungufu mbalimbali kama kuomba kuwezeshwa wakati biashara sio za kwao, kutokuwa na biashara inayoendelea nk.
        Shelukindo alisema “Ni jambo jema kwamba wajasiriamali wetu wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, wako wajasiriamali katika fani tofauti pia kama Mafundi wa kushona nguo za aina tofauti,  mafundi seremala, magari nk wako pia wajasiriamali wa kusindika vyakula, ufugaji wa samaki, ufugaji wa kuku, kutengeneza mizinga ya nyuki nk, wako wajasiriamali katika biashara za vyakula, kuuza vinywaji, umeme jua, teknolojia ya mawasiliano nk”.
        Bwana Shelukindo aliwataja wajasiriamali waliomaliza mafunzo na watapatiwa ruzuku ya vitendea kazi ili kupanua biashara zao. Katika kituo cha Dar Es Salaam wajasiriamali walifaulu ni Catherine Urio, Josephine Kisiri, Zainabu Juma Zayumba, Elizabeth Chami, Richard Kwiligwa, Hilary Meck Mremi, Damas Daniel Msoka, Innocent Mbelwa, Stumai Namanga, Martin Richard Tupilike, Dasina J Buzuka, Christabela Lymo, Dadan J Munisi, Faraji Bakary Mgwegwe, Issa Lema na Valerian Tigano Luzangi. Shelukindo aliwataja pia washindi wa kituo cha Arusha kuwa ni Ansilla Danny, Bibie Msumi, Rogers Msangi, Simon Kinabo, Sophia Khalfan, Yuda Mbando, Amani Lymo, Adam Akilinyingi, Joseph M. Mnemwa, Rose Tesha na Victoria Riwa.
       Aliendelea kuwataja wajasiriamali waliofaulu katika kituo cha Mwanza ambao ni Bora Mganda, Brighton Dismas Maricell, Mangana Kilahanya Kigombe, Prudence Mubito, Musa Mahushi George, Innocent K. Doi, Amos Edward Mwambola, Edith Mudogo, Aron Magembe, Yusuph A. Kawaga, Zamda Shabban, Oscar Bosco Kabobo, Yahaya Fundisa, Dainess Ngaiza na Boniface Joseph Minja. Na katika kituo cha Mbeya wajasiriamali waliofaulu kupata ruzuku baada ya mafunzo ni Rose Eliudi Maruila, Benedict Abel Matandiko, Vumilia Mtweze, Bahati Mbata, Hellen A. Mwanguku, Felix Phillip Kamuhabwa, Festo Mwakasege, Phares Richard Lymo, Iradi A. Msemwa, Gabriel Mwalugaja na Tatu Ngemela. Jumla ya ruzuku ya vitendea kazi vya thamani ya shilingi milioni 200 vitatolewa kwa wajasiriamali hawa. 
        Bwana Shelukindo aliendelea kusema “Safari Lager tunayofuraha kubwa kuwasaidia wajasiriamali hawa, tunawapa pongezi kwa uvumilivu wao na jitihada kubwa waliyo nayo. Tutawakabidhi vitendeakazi vyao katika hafla maalumu kuanzia wiki mbili zijazo”. 
        Akielezea mafunzo yalivyoendeshwa Bw. Joseph Migunda wa taasisi ya TAPBDS alisema wajasiriamali katika mikoa yote wameonyesha uelewa kwa kiwango cha juu na wote walifaulu mtihani wa kuhitimisha mafunzo hayo. Alisema “Tuna imani wajasiriamali watatumia elimu na ruzuku wanayopatiwa ili kupiga hatua zaidi kufikia ndoto zao”.
       Bwana Shelukindo alimaliza kwa kuwashukuru watanzania wote kwa kushiriki shindano hili, aliendelea “Shukrani nyingi sana ziende pia kwa wanywaji wetu wa bia ya Safari Lager, bila wao hakika zoezi zima la Wezeshwa na Safari Lager lisingewezekana, tunawaomba waendelee kufurahia bia yetu”. Aliwaomba radhi wajasiriamali ambao hawakufaulu, na wale wanaoendelea kutuma fomu wasitume tena, wajiandae kushiriki shindano lijalo la Wezeshwa na Safari Lager baadae mwaka huu.
______________________________________________________________________
Kuhusu Wezeshwa na Safari Lager;
Ni shindano linaloendeshwa na bia ya Safari Lager, likiwa na lengo la kuwainua wajasiriamali wadogowadogo kwa kuwapa msaada wa ruzuku ya vitendea kazi. Kwa maelezo zaidi tembelea www.wezeshwa.co.tz

Kwa Maelezo zaidi wasiliana na:
Oscar Shelukindo, Safari Lager Brand Manager, simu;  +255 767 266 833, [Oscar.Shelukindo@tz.sabmiller.com].
Kuhusu TBL
Tanzania Breweries Limited (TBL) inatengeneza, kuuza na kusambaza bia, vinywaji vyenye ladha ya matunda vilivyo na kilevi na vinywaji visivyo na kilevi hapa Tanzania. TBL pia ndiyo kampuni mama ya Tanzania Distilleries Limited pamoja na kampuni shiriki ya Mountainside Farms Limited.

Bia zinazotengenezwa na kampuni ya TBL ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Lager, Vinywaji vingine vinavyotengenezwa na kundi la makampuni ya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redd’s Premium Cold na Grand Malt.

Kundi la makampuni ya TBL limeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam, limeajiri watu wapatao 1,300 na linawakilishwa nchi nzima na viwanda vinne vya bia, kiwanda kimoja cha kutoneshea, kimoja cha kutengenezea kimea pamoja na bohari nane za kusambazia bia.

Kuhusu SABMiller
SABMiller plc moja kati ya makampuni makubwa ya bia duniani ikiwa na mikataba ya kutengeneza na kusambaza bia kwenye nchi zaidi ya 60 katika mabara matano. Bia zake ni pamoja na zile za kimataifa kama Miller Genuine Draft, Peroni Nastro Azzurro na Pilsner Urquell vilevile na bia nyingine zinazoongoza kwenye masoko ya ndani ya nchi mbalimbali. Nje ya Marekani, SABMiller ni moja ya kati ya makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji vya Coca-Cola duniani. Hivi karibuni SABMiller plc ilinunua kampuni ya bia ya Foster’s pamoja na shughuli zake za uzalishaji nchini India. SABMiller imeorodheshwa kwenye masoko ya hisa ya London na Johannesburg.


No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages