Breaking News

Your Ad Spot

May 27, 2012

ARUSHA WAFUNIKA RUAHA HALF MARATHON 2012

IRINGA
WAKAZI wa mjini Iringa mwishoni mwa wiki walishuhudia kwa mara ya kwanza wanariadha zaidi ya 320 wakichuana katika mbio za barabarani za Ruaha Half Marathon huku wanariadha kutoka mkoani Arusha wakitawala.
       Katika mbio hizo, zilizoanzia mnara wa saa karibu na ofisi za Manispaa ya Iringa na kuelekea njia ya kwenda Ruaha National Park na kurudi hadi uwanja wa Samora  ambako zilihitimishwa, kwa upande wanaume Alphonce Felix kutoka sekondari ya Winning Spirit alishika nafasi ya kwanza akitumia saa 1:03.09 huku kwa wanawake, Mary Naali kutoka klabu ya Skytel akishinda kwa saa 1:13.01.
      Alphonce alifuatiwa na Dickson Marwa wa klabu ya Mbui ya jijini Dar es Salaam 1:03.29 huku nafasi ya tatu ikikamatwa na Saidi Makula wa Winnig Spirit 1:03:29 mshindi wa nne Getuni Tsekeway pia wa Arusha 1:04.06 wakati aliyefunga tano bora alikuwa ni mwenyeji, Moses Mwadeni aliyetumia saa 1:11:18.
      Naali ambaye kwa muda huo kaweka rekodi kwa wanawake hapa nchini, alifuatiwa kwa mbali na Stephancy Perkins kutoka Australia aliyetumia saa 1:32.55, Natali Struble wa Marekani alishika nafasi ya tatu kwa saa 1:38.50 huku nafasi ya nne ikienda kwa Yoko Imamura wa Japan 1:59.00 wakati Mia Mjengwa wa Iringa alifunga tano bora akitumia saa 2:03.00.
       Mbio hizo, ambazo zimepangwa kufanyika kila mwaka Jumamosi ya mwisho wa Mei, kwa mwaka huu wa kwanza zilishirikisha wanariadha chipukizi wengi kutoka Iringa na mikoa za jirani na baadhi wa kimataifa wa hapa nchini na kutoka nje. Ruaha Half Marathon, iliratibiwa na kudhaminiwa na shirika lisilo la kiserikali
la Mindset Empowerment (ME), lenye makao yake makuu mjini Iringa, zikiwa na ujumbe wa kulinda na kuboresha mazingira, ambako kauli mbiu yake ikiwa ni 'Mazingira bora kwa utalii endelevu, Okoa mto Ruaha’.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages