Na Rose Jackson ,Arusha
Benki ya Eco kwa kushirikiana na shirika la uwekezaji wa sekta ya umma la Afrika ya Kusini(PIC) imetia saini mkataba ambayo imegarimu kiasi cha dola za Kimarekani Milioni 250 kwa ajili ya kukuza na kuimarisha shuguli mbalimbali za Miradi ndani ya nchi za bara la Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwekeana saini ya mkataba huo Mkurugenzi wa Eco Benki Bw Anolrd Ekpe alisema kuwa kuanzia sasa zoezi la kuwekeza miradi mbalimbali kwa nchi za bara la afrika zinaanza rasmi.
Alifafanua kuwa mpango huo ambao unaanza kwa nchi za bara la Afrika utakuwa na nafasi kubwa sana ya kuweza kuruhusu uwekezaji wa hali ya juu sana huku hata baadhi ya benki ikiwemo hiyo ya Eco Benki kuweza kukua na uimarika kiuchumi
Pia alisema kuwa kupitia makubaliano hayo baina ya benki hiyo na PIC pia kutaweza kuongezeka sana kwa shuguli mbalimbali za uwekazaji katika bara la Afrika hali ambayo nayo itachangia sana kukua kwa uchumi ambapo ndilo lengo halisi la makubaliano hayo
“huu mpango ambao utaenda kwenye nchi 32 za bara la Afrika zitaweza kutumia vema mkataba huo ambapo kupitia hata mpango huo uchumi nao utaaimarika sana na hata kiwango cha uwekezaji nacho kitapanda tofauti na sasa ndani ya nchi hizo”aliongeza Bw Anorld
Awali alifafanua kuwa kupitia mchakato huo wa nchi 32 za bara la Afrika nayo Eco Benki itaweza kunufaika sana kwa kuwa mapato yake nayo yataweza kuongezeka kwa kiwango cha asilimia 19.58 hali ambayo nayo ni nzuri kwa ajili ya shuguli mbalimbali za uwekezaji wa bara la Afrika.
Bw Anorld alisema kuwa ili kuweza kuimarisha hata uchumi wa nchi mbalimbali za bara la Afrika wamejiwekea Mikakati maalumu wa kuhakikisha kuwa kila jamii inafikiwa na huduma muhimu kwa ajili ya kukuza na kuimarisha uchumi ambao ndio lengo halisi la Benki hiyo
Alitaja Mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa benki hiyo inajikita zaidi kwenye kila kona ya nchi ambapo kupitia kona hizo wataweza kuwekeza kwa kiwango cha hali ya juu sana hali ambayo nayo itachangia kukua na kuimarika kwa uchumi barani Afrika.
Your Ad Spot
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269