| Iddi Simba akisindikizwa na Polisi kwenda kizimbani |
Amefikishwa mahakamani pamoja na washtakiwa wengeni watatu, Mkurugenzi wa shirika hilo, Salim Mwaking’inda na Meneja Mkuu wa shirika hilo Victor Milanzi.
Katika kesi hiyo, washitakiwa wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Alex Mgongolwa na Said El Mamry na upande wa Serikali unawakilishwa na wakili wa Taasisis ya Kuzia na Kupambana na Rushwa,Ben Lincol.
Mbele ya Hakimu Mfawidhi Ilivin Mugeta ,wakili Lincoln alisema katika mashtkama manane yanayowakabili, la kwanza kula njama ambalo linamkabili Simba na Milanzi ambao inadaiwa, kati ya Septemba 2 ,2009, jijini Dar es salaam walikula njama na watu wasiofahamika na kutenda kosa hilo kinyume na kifungu cha namba 29 cha Sheria ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa ya mwaka 2007.
Shitaka la tatu ni la kuhamisha fedha kinyume na kifungu cha 29 cha Sheria ya kupambana na Rushwa, kwamba Simba na Milanzi kwa tarehe hiyo Simba akiwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Milanzi akiwa Meneja Mkuu wa UDA, kwa pamoja walishirikiana kuhamisha fedha kwa faida yao binafsi sh milioni 320,ikiwa ni malipo ya awali na ni sehemu ya ya malipo ya hisa za UDA ambazo walizipokea wao binafsi kupitia nyadhifa zao .
Washitakiwa wote wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti na Kesi hiyo imeairishwa hadi Juni 28 mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa.
Iddi Simba akiwa na wakili El Maamry (kushoto) mahakamani
Mwaking'inda Picha kwa hisani ya BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269