.

RAIS KIKWETE AZINDUA BLOGU NA TOVUTI RASMI YA CCM

May 14, 2012

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jaklaya Kikwete akizindua Blogu hii na Tovuti  Rasmi vyote vya Chama, hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo. Wanaomwelekeza ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye na Suleyman Mwenda ambaye ni Mkuu wa masuala ya Teknolojia Mawsiliano, Idaya ya Mawasiliano na Umma Makao Makuu ya CCM. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) John Chiligati na Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar) Vuai Ali Vuai. Tovuti ya CCM ni www.ccm.or.tz kuiona Tovuti hiyo  BOFYA HAPA na Blogu BOFYA PIA HAPA
Nape akimweleza Rais Tovuti na Blogu vinavyofanya kazi za Chama
Nape akimshauri jambo Rais Kikwete Kushoto ni Makamu wa Rais Dk. Mohamed Graib Bilal, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Sheni na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Amani Abeid Karume
 Rais Kikwete na Mwenyeji wake katika shughuli hiyo, Nape wakiingia kwenye eneo la uzinduzi  huo
 Nape akitoa maelezo mafupi kuhusu faida ya CCM kuwa na Tovuti Ramsi na Blogu
 Katibu Mkuu Wilson Mukama akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM kuzindua tovuti na blogu hiyo
 Kisha Nape akapanda jukwaani kuporomosha muziki na bendi ya Siper Melody, akapagawisha watu
 Katibu wa NEC, Oganaizesheni Asha Abdallah Juma akimpongeza Nape  kwa uhodari wa kucharaza gita.
 Makongoro Nyerere ambaye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara akimpongeza
 Watu wakajimwaya mwaya uwanjani
 Miduara kwa sanaaaaaa
 Baadhi ya wajumbe wa NEC wakisakata muziki
 Mzee Mtandika akakumbuka enzi hizo
 Rais akiondoka ukumbini
BYEEEEEEEE!!!!! Rais akasema

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª