Breaking News

Your Ad Spot

May 20, 2012

YANGA KWAWAKA LEO, WANACHAMA WATANGAZA KUMTIMUA NCHUNGA


 Mwenyekiti wa Kamati ya Wazee wa Klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali akitangaza kumfuta Uenyekiti wa timu hiyo, Lyod Nchunga, wakati wa mkutano wa wanachama unaoendelea muda huu kwenye klabu hiyo, Mtaa wa Jangwani/Twiga jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa Yanga wakishangilia tamko la kumg'oa Mwenyekiti wa Klabu hiyo Lyod Nchunga
 Mashabiki wa Yanga ambao si wanachama, wakifuatilia mkutano wakiwa mbali
 Tofauti na vikao vingine vya Yanga ambavyo hufanyika katika ukumbi wa  jengo la Klabu hiyo, mkutano huu wa leo unafanyika kwenye Uwanja nje ya jengo.
 Mmoja wa wanachama wa Yanga, anayeitwa Nyachia akionyesha kadi yake wakati wa kujisajili kuingia kwenye mkutano huo. Picha zote na Nkoromo Daily Blog: Fuatilia katika Blogu hii baadaye tunapandisha Video ya sehemu ya mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages