Breaking News

Your Ad Spot

Jun 18, 2012

KAMPENI YA WAJANJA WA VODACOM YAZINDULIWA DAR

DAR ES SALAAM
Kampeni ya wajanja wa Vodacom imezinduliwa kwa mafanikio makubwa katika fukwe za Coco beach.
    Kampeni hiyo inayofanywa na kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom, itafanyika katika Mikoa mbalimbali ya Tanzania ikiwemo Morogoro, Mtwara, na Tanga ikiwa na lengo la kuwahamashisha vijana ambao ndio nguzo ya Taifa kufurahia huduma nzuri zinazotolewa na kampuni hiyo kwa ajili yao.
    "Kampeni hii maalum kwa vijana ina lengo la kuongeza uelewa kuhusu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kwa vijana katika kuwarahisishia mawasiliano". Alisema Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni hiyo Rene Meza na kuongeza;
    “Kupitia kampeni hii tunawahamasisha vijana na jamii yote kwa ujumla kujumuika pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, wako huru kutoa maoni na kupewa majibu kuhusu bidhaa na huduma zinazotolewa”. Alisema Rene Meza.
     Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa amesema kuwa kampeni hiyo imedhamilia kuwainua vijana katika masuala mbalimbali pamoja na kuwapa wasanii chipukizi nafasi ya kuonesha vipaji vyao.
   “Kampeni hii ya wajanja wa Vodacom inawapa fursa vijana kuonyesha vipaji vyao kama ambavyo siku ya leo umeona vijana mbalimbali wamepanda jukwaani na kuimba”
     Kampeni ya Wajanja wa Vodacom imetoa nafasi kwa wateja wa mtandao huo kutumia facebook na twitter bure, kutuma ujumbe mfupi wa maneno mitandao yote kwa
shilingi 25 na kupiga simu kwa shilingi moja kwa sekunde kuanzia saa nne usiku
hadi saa kumi na mbili asubuhi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages