Breaking News

Your Ad Spot

Jun 6, 2012

WABUNGE BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI WAAPISHWA

 Saamweli Sitta
 Alhaji Adam Kimbisa
 Angela Charles Kizigha
 Bernard Musomi Muruyana
 Abdullah Ali Hassan Mwinyi
 Nderkindo Kessy
 Makongoro Nyerere
 Twaha Issa Taslima
Shy Rose Bhamji

HABARI AKWA UFUPI

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA)  wameapishwa rasmi kushika madaraka hayo huku Tanzania ikiwa na Wawakilishi tisa katika Bunge hulo.

Wabunge hao waliapa baada ya kupatikana Spika wa mpya wa Bunge hilo ambapo safari hii ikiwa ni Uganda kushika Uongozi huo wa Juu wa Bunge na Mwana Uchumi, Margareth Ziwa kuchukua nafasi hiyo.

Wabunge wote wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Mashariki waliokula kiapo hii leo ni pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge EALA, Alhaj Adam Omar Kimbisa na Katibu wake, Mh Shy-Rose SaddrudinBhanji.

Wengine ni Mhe. Anjela Charless Kizigha, Mh. Maryam Ussi Yahya,Mh.Nderkindo Perpetua Kessy, Dkt Twaha Issa Taslima, Mhe. Abdullah Ali Hassan Mwinyi, Mhe Bernard Musomi Murunyana Mhe. Charles Makongoro Nyerere na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta anaeingia kwa wadhifa wake wa Uwaziri.

Wabunge hao wameapisha pamoja na wabunge wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi  (source- Father Kidevu Blog)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages