Breaking News

Your Ad Spot

Jun 22, 2012

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WATIMULIWA KWA ULAFI, WENGINE WABURUZWA MAHAKAMANI

Waziri Mkuu Mizengo Pinda
DODOMA, TANZANIA
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amewavua madaraka wakurugenzi wanane wa Halmashauri  huku wawili kesi zao zikifikisha mahakamani.
   Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Waziri wa Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Serikali Hawa Ghasia alisema wengine watatu wamepumzishwa kazi na kuongeza kuwa maamuzi ya kufuta kazi wakurugenzi hao yalifanyika katika kipindi cha mwaka 2011/12.
    Alisema kufuatia tuhuma mbalimbali za ubadhilifu wakurugenzi wawili ambao ni Harold Senyagwa ( Kyela) na Rhoda Nsemwa (Bagamoyo) kesi zao zipo mahakamani na kwamba wakati hayo yakijiri Waziri Mkuu ameteuwa wakurugenzi wengine wapya 14 kujaza nafazi zilizokuwa wazi na wengine 22 wamwehamishwa vituo huku 11 wakipewa onyo kali.
   Waziri Ghasia alisema sababu ya kuwavua madaraka  wakurugenzi wanane ni kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao na kwamba wakurugenzi hao kwa sasa wamepewa kazi zingine katika halmashauri hizo .
    Aliwataja waliovuliwa madaraka kuwa ni pamoja na Consolata Kamuhambwa (Karagwe), Ephraim Kalimalwendo (Kilosa), Elly Mlaki (Babati), Eustach Temu (Muheza) na Jacob Kayange ( Ngorongoro).
   Wengine ni Hamida Kikwega (Chato), Majuto Mbuguyu ( Jiji la Tanga) ma Raphael  Mbunda (Arusha Manispaa ).
     Waziri Ghasia alisema kwa sasa serikali ipo katika mchakato wa kujaza wakurugenzi katika Halmahsuari ambazo hazina watendaji hao.
    Alisema orodha ya wakurugenzi hao imeshapelekwa kwa Rasi Jakaya Kikwete na inatarajiwa hadi Julai Halmashauri nyingi zitakuwa na wakurugezni wake.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages