Breaking News

Your Ad Spot

Jul 26, 2012

ASKOFU MKUU RUGAMBWA AMTEMBELE RAIS KIKWETE IKULU

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amekutana na kufanya mazungumzo na Askofu Mkuu Protase Rugambwa ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Baba Mtakatifu Benedict wa XVI kuwa Katibu Mwambata wa Idara au Kongregasio ya Uenezaji wa Injili kwa ajili ya Mataifa na Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari yenye makao yake, Roma. Wakati wa mazungumzo hayo Rais Kikwete kwa mara nyingine tena,amempongeza Askofu Rugambwa kwa uteuzi wake na kusema kuwa uteuzi huo ni kielelezo dhahiri cha imani kubwa aliyonayo Baba Mtakatifu kwa askofu huyo na kuwa ni heshima kubwa kwa Mtanzania kupata nafasi ya kushika wadhifa huo mkubwa. Kabla ya Uteuzi huo Askofu mkuu Rugambwa alikuwa askofu wa jimbo Katoliki Kigoma. Pichani, Rais Kikwete akiagana na Askofu Mkuu Rugambwa bada ya mazungumzo yao.(Picha na Freddy Maro) PICHA HII IPO PIATANZANIA VISION BLOG

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages