Breaking News

Your Ad Spot

Jul 19, 2012

MAPYA AJALI YA MELI ZAINZIBAR: MAOMBOLEZO SIKU TATU NCHI NZIMA,130 BADO HAWAJAPATIKANA, SHUGHULI ZA BUNGE ZAAHIRISHWA DODOMA

Akizungumza asubuhi hii, kabla ya Spika wa Bunge Anna Makinda kutangaza kuasitishwa shughuli za bunge leo hadi kesho, Waziri wa Nchi, Uratibu na Bunge, William Lukuvi amesema, Siku tatu za maombolezo zilizotangazwa kufuatia ajali ya meli iliyotokea Zanzibar, zimetangazwa pia kwa Tanzania Bara.
       Amesema  taarifa ambazo bunge limepata, meli hiyo ya  Star Gig ilikuwa na watu 250 wau wenye umri wa watu wazima 250 wakiwemo wafanyakazi tisa wa meli hiyo.
      Lukuvi amesema, hadi asubuhi hii waliookolewa wakiwa hai ni  watu 149, walokufa 31 na wote wametambuliwa na ndugu na jamaa zao.
   Amesema miongoni mwa walionusurika wamo watalii 14  na kwamba watalii wengine wawili ni miongoni mwa ambao hawajapatikana hadi sasa
     Lukuwi amesema kwa kuwa meli ilikuwa inatoka Dar es Salaam, kuna uwezekano wa kuwepo watu waliokpatwa na mkasa huo ambao  ni wakazi wa Tanzania Bara, hivyo ndigu au jamaa watakaokuwa wakifuatilia taarifa, kituo cha Mawasiliano kimewekwa Ofisi ya Mkuu ya wa mkoa wa Dar es Salaam.
 Wakati huohuo, imeelezwa kwamba mazishi yamenaza kufanywa Zanzibar na ndugu jamaa waliowapata ndugu zao, Hata hivyo kwa mujibu wa Spika Makinda kuna uwezekano wa kufanyika mazishi ya halaiki kutokana na kwamba idadi ya ambao hawajapatikana badi ni kubwa.
   Akiahirisha Bunge, Makinda amesema wabunge wametoa posho yao ya leo kwa ajili ya maombolezo ya msiba huo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages