Breaking News

Your Ad Spot

Jul 21, 2012

UN YAOMBOLEZA MAAFA YA KUZAMA MELI ZANZIBAR

 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Jan Eliasson akisaini kitabu cha Maombolezo ambacho kimefunguliwa katika Ubalozi  wa  Kudumu wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania katika Umoja wa  Mataifa.  Katika Salamu zake, Naibu Katibu Mkuu ameelezea kuguswa kwake na tukio la ajali  ya kuzama kwa meli  na  hasara iliyotokana na ajari hiyo ikihusisha pia kupotea kwa maisha ya watu. Mhe. Jan Eliasson ni miongoni mwa wanadiplomasia ambao wamekuwa wakifika kutoa salamu zao za pole na kuungana na watanzania katika kipindi hiki cha majonzi.
Naibu Katibu Mkuu  wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Jan Eliasson akizungumza na Kaimu Balozi, Dkt. Justin Seruhere mara baada ya kusaini kitabu cha  maombolezo ambapo   alielezea  namna gani anavyoifahamu Tanzani na mapenzi yake makubwa kwa nchi hiyo  na kwamba ni kama miaka miwili tu iliyopita alikuwa Kisiwani Zanzibar.   Katika salamu zake za pole  Mhe.  Elliasson amesema sala na dua zake anazielekeza kwa wahanga wa tukio hilo,  Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kwamba Umoja wa Mataifa uko pamoja na watanzania katika  kipindi hiki kigumu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages