Breaking News

Your Ad Spot

Aug 4, 2012

KATIBU WA CCM TAWI LA NORTH LONDON AJITOSA UCHAGUZI UVCCM, TAIFA

DAR ES SALAAM, TANZANIA
KADA  wa  Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) na Msomi wa  digrii ya uchumi, Neema Kumba, amejitosa kwenye uchaguzi mkuu wa umoja huo Taifa kwa kuchukua kugombea nafasi ya NEC na uwakilishi UWT.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema jana, Agosti 3, jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na Mkuu wa Idara ya Oganizesheni na siasa UVCCM, Taifa, Sophia Duma,

Kumba ambae awali alikua Katibu wa CCM, tawi la North London, Nchini Uingereza, alipokua akichukulia digrii yake ya uchumi, alisema lengo ni kuakikisha mikakati thabiti  inajengeka kwa  kiwango kikubwa miongoni mwa vjana na wanawake wote nchini.

“Kwa umakini wangu na maarifa niliyoyapata kwenye elimu na uwepo wangu ndani ya chama, ndani na nje ya nchi, ni wakati sasa na mimi kuwasaidia wenzangu hasa Vijana na wanawake ambao mara nyingi wamekua wakisahauriwa  na huu ndio wakati wa kuwainua” alisema Kumba.

Mbali na kuchukua fomu hiyo ya NEC na uwakilishi UWT, Taifa, pia tayari alisha chukua fomu ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti Uvccm, Wilaya Ilala.

Mpaka sasa tayari wanachama mbalimbali wa UVCCM, wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania uongozi ambapo mwisho wa kurudisha fomu hizo, Agosti 6.
Neema akikabidhiwa fomu jana na Sophia Duma Makao Makuu ya UVCCM jijini Dar es Salaam .

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages