Breaking News

Your Ad Spot

Aug 5, 2012

MKUU MKOA WA SINGIDA DR. KONE ATEMBELEA WIZARA YA FEDHA KATIKA MAONYESHO YA WAKULIMA YA NANENANE MJINI DODOMA

 Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr.  Parseko Kone (kushoto) akitaka kujua  maoni kutoka kwa   Mhasibu wa Wizara ya Fedha Abbas Myeto(kulia)kuhusu taratibu za kupata pesheni kwa watumishi wa umma wanapostaafu . Mkuu huyo wa Nkoa wa Singida aliomba ufafanuzi huyo leo alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonyesho ya wakulima kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr.  Parseko Kone (kushoto) akitaka kujua jana mjini Dodoma kutoka kwa watendaji wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) kwanini kuna utofauti wa ubora katika bendera ya Taifa ya kuweka katika magari kwa viongozi. Mkuu Mkoa huyo aliuliza swali hilo leo alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonyesho ya wakulima kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma. Aliyeshika bendera ndogo ya taifa ni Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Mikataba Maalum Modecai Mato (kulia).
 Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr.  Parseko Kone (kushoto) akipata maelezo mafupi  jinsi  Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini [GPSA] inavyosaidia katika kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma yaliyokuwa yakifanyika kupitia ununuzi wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya ofisi za serikali na taasisi zake. Mkuu Mkoa huyo alipata maelezo hayo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Mikataba Maalum Modecai Mato (kulia)  jana  alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonyesho ya wakulima kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma.
 Mchambuzi wa Mifumo ya Komputya Mkuu Daraja la III kutoka Idara ya Menejimenti ya TEKNOHAMA ya kifedha , Wizara ya Fedha Margethi Ambrosi Nembo (kushoto) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr.  Parseko Kone (kulia) leo mjini Dodoma jinsi kuingiza mishahara na malimbikizo ya watumishi wa umma kwa kutumia TEKNOHAMA . Mkuu Mkoa huyo alikuwa katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr.  Parseko Kone (kushoto) akitoa changamoto kwa watumishi wa Chuo cha Mipango cha Dodoma kuwa na mitaala ambayo itawaandaa wananchi kuanzia ngazi ya chini juu ya kuwa na mipango mizuri ya matumzi bora ya ardhi ili kukabiliana na ongezeko la watu nchini. Mkuu Mkoa huyo alitoa kauli hiyo leo mjini Dodoma alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dodoma

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages