.

MWANDISHI WA HABARI AFARIKI DUNIA ZANZIBAR

Aug 4, 2012

MWANDISHI WA HABARI WA SHIRIKA LA MAGAZETI YA SERIKALI HALIMA ABDALLA OMAR, AMEFARIKI  DUNIA  LEO ASUBUHI HUKO NYUMBANI KWAO MIEMBENI  MJINI  ZANZIBAR.

MFANYAKAZI HUYO ALIZIKWA JANA KATIKA MAZISHI YAKE YALIYOFANYIKA KATIKA MAKABURI YA MWANAKWEREKWE YALIYOPO WILAYA YA MAGHARIBI.

HALIMA ALIAJIRIWA NA SHIRIKA LA MAGAZETI YA SERIKALI OKTOBA 18 MWAKA 2008, BAADA YA KUHITIMU MAFUNZO YA UANDISHI WA NGAZI YA CHETI KATIKA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI ZANZIBAR.

MWAKA 2011, MWANAHABARI HUYO ALIJIUNGA NA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI ZANZIBAR , KWA MASOMO YA STASHAHADA KABLA YA KUAHIRISHA MASOMO KWA SABABU ZA UGONJWA.

HADI KUFARIKI KWAKE, HALIMA ALIKUWA MFANYAKAZI WA SHIRIKA LA MAGAZETI YA SERIKALI NA MWANAFUNZI KATIKA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI ZANZIBAR.

HALIMA ALIZALIWA JUNI 8 MWAKA 1984 NA KUISHI NA WAZEE WAKE JANG’OMBE MJINI HAPA NA ALIMALIZA MASOMO YAKE KATIKA SKULI MASASI MWAKA 2004 NA KUJIENDELEZA KATIKA SKULI YA HAMAMNI AMBAPO ALIMALIZA MWAKA 2006.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª