.

NAPE AFUTURISHA WAJUMBE WA NYUMBA KUMI MKOANI MOROGORO

Aug 17, 2012

 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akikaribishwa na Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Sixtus Mapunda na Kada wa CCM Hassan Bantu (kulia) alipowasili kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya Forest ambako aliandaa futari kwa ajili ya mabalozi wa nyumba kumi na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali wa  CCM kutoka wilaya za mkoa wa Morogoro jioni hii ya leo Agosti 17, 2012.

 Nape akihutubia baada ya kufuturisha
 Nape akihutubia huku wazee wakimsikiliza kwa makini.
 Sheik  Khamis Ali Mbilikila akisoma dua baada ya futari hiyo iliyoandaliwa na Nape kwenye ukumbi wa Shule ya sekondari Forest mjini Morogoro.
 Nape akishiriki kuomba dua baada ya futari. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro
 Kina mama wakishiriki kuomba dua baada ya futari
 Kina baba wakiomba dua baada ya futari hiyo
 Nape, Bendera na Kingu wakiwa wamesimama baada ya futari hiyo.
 Badhi ya waalikwa wakimshukuru Nape kwa kuandaa  futari hiyo
 Nape na mbunge wa zamani, Semindu Pawa wakifurahia jambo baada ya kuonana kwenye futru hiyo
 Nape akiagana na mjumbe wa nyumba kumi  Zuberi Fikirini baada ya futari. Mjumbe huyo ni mlemavu wa miguu
 Kwanza Nape alikutana na mkuu wa mkoa wa zamani wa Morogoro Steven Mashishanga wakasalimiana kwa furaha na bashasha ya hali ya juu
 Waumini walisali kwanza kabla ya futari
 Kisha wakajumuka kufuru
 Mashishanga, Fikiri juma wa mjini,Nape na wa mkoa petro kingu wakifuturu, futari iliyoandaliwa na Nape kwenye ukumbi wa Shule ya sekondari Forest mjini Morogoro.
 Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Sixtus Mapunda na Msaidizi wa  Katibu NEC, Itikadi na Uenezi, Taifa, Okctavian wakifuturu
 Babu akijisevia futari, wakati wa futru hiyo iliyoandaliwa na Nape kwenye ukumbi wa Shule ya sekondari Forest mjini Morogoro.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel; Bendera akijinafasi wakati wa futru hiyo
 Kina mama wakifuturu
Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda akimshukuru Nape kwa kuandaa futari hiyo

5 Comments:

Anonymous said...

ndugu wananchi msidanganywe kwa pipi wakati wenzenu wanakula keki, tunataka usawa ktk kila ngazi kuanzia ya chini mpaka ya juu , sio kufuturishana kwa danganya toto

Bashir Nkoromo said...

Tunashukuru kwa maoni yako, je wengine mnasemaje?

Anonymous said...

CCM IMEONESHA NJIA VYAMA VINGINE VINAPASWA KUIGA MFANO HUU...NAPE AMEWAUNGA MKONO NDUGU ZETU WAISLAMU KATIKA MFUNGO HUU WA RAMADHANI...

Anonymous said...

Huyo jamaa anayesema eti futari ni danganya toto namshangaa sana! lakini namuomba Ndugu Nape na Chama Cha Mapinduzi kwa jumla asife moyo maana watu hawawezi kukusifu kwa kila jambo hasa kama linakujenga kisiasa.

Anonymous said...

Mbona sasa mmefuturiosha huko Morogoro tu, kulikuwa na agenda gani muhimu kuliko kwingine?

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª