Breaking News

Your Ad Spot

Aug 9, 2012

RAIS AWAAPISHA WATENDAJI WA MAHAKAMA

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amemwapisha Mtendaji Mkuu wa Mahakama pamoja na Msajili mkuu wa Mahakama na msajili wa mahakama ya rufani katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam. Walioapishwa leo ni Mtendaji mkuu wa Mahakama Bwana Hussein Katanga,Msajili Mkuu wa Mahakama Bwana Ignus Paul Kitusi na Msajili wa Mahakama ya Rufani Bwana Panterine Muliisa Kente.Pichani Mtendaji mkuu wa Mahakama Bwana Hussein Katanga akila kiapo mbele ya Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue(kushoto) pamoja na maofa waandamizi wa mahakama aliowaapisha leo asubuhi ikulu jijini Dar es Salaam.(Wapili kushoto) ni Mtendaji mkuu wa Mahakama  Bwana Hussein Katanga,(Wanne kushoto) ni Msajili Mkuu wa Mahakama Bwana Ignus Paul Kitusi na kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufani Bwana Panterine Muliisa Kente(picha na Freddy Maro)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages