.

ULIMBOKA AREJEA NYUMBANI

Aug 12, 2012

Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka, akiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mjini Dar es Salaam, baada ya kuwasili kutoka nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuumizwa  na kundi la watu waliomteka na kumpiga kwenye msitu wa Mabwe Pande, wilaya ya Kinondono, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Akizungumza baada ya kurejea na kulakiwa na kundi la wanachama wa Chama hicho cha Madaktari waliokuwa wakiimba wimbo wa vyama vya wafabyakazi wa "Solidality for rever", ulimboka alisema afya yake imeimarika na ni mzima wa afya na anamshukuru . "Namshukuru Mungu, nimepona na sasa ninao uwezo wa kufanya chochote" alisema D. Ulimboka bila kufafanua zaidi.


Hali ya  Dk. Ulimboka alipokuwa amelazwa MOI jijini Dar es Salaam, baada ya kipigo

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช