.

MBIO ZA MWENGE ZAPATA AJALI BUNDA

Aug 18, 2012


BUNDA, TANZANIA
ZAIDI ya watu 15 wakiwemo waandishi wa habari, leo wamenusurika kifo, baada ya magari matatu yaliyokuwa kwenye msafara wa Mwenge wa Uhuru kugongana wilayani Bunda, mkoani Mara.

Katika tukio hilo magari mawili yameharibika vibaya, likiwemo la taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) walilokuwa wamepanda pia waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari, akiwemo mwandisi wa habari hizi.

Mashuhuda wa tukio hilo wametuambia kuwa chanzo cha ajali ni mwendo kasi, ambapo gari moja mali ya halmasauri ya wilaya lenye namba za usajili SM 8809, iligonga kwa nyuma gari ya TAKUKURU yenye namba za usajili T. 645 BCT.

Hali hiyo ilisababisha magari mengine kugongana na kuaacha njia likiwemo la TRA lenye namba za usajili STJ 9663, ambapo pia kama zisingekuwa juhudi za madereva wa magari mengine kufanya jitihada za makusudi kwa kuacha barabara na kuingia upande mwingine uhenda ingekuwa ajali kubwa sana.

Katika tukio hilo kakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa, ambapo baadhi yao wamepata maumivu ya kawaida tu.

Polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa ajili hiyo iliyotokea majira ya jioni katika kijiji cha Kasahunga, kwenye barabara kuu ya Bunda-Ukerewe, wakati msafara wa mwenge huo ukielekea kwenye mkesha katika kijiji cha Kibara, baada ya kuzindua na kuweka mawe ya misingi kwenye  miradi 9 ya maendeleo iliyogarimu zaidi ya sh. bilioni 1.4.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช