Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Dk. Seif Rashid (Kulia) akisalimiana na akina mama wa Kijiji cha Mtanza baada ya kumalizika kwa mkutano na wananchi wa eneo hilo wakati wa ziara ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge pamoja na kuwaeleza majukumu mengine aliyonayo sasa ya unaibu waziri.
Dk Rashid akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mtanza jimboni humo juzi. Kulia ni Diwani wa Kata ya Mwaseni, Athuman Mbange (CUF) na kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtanza. |
Akina mama wa Kijiji cha Mibuyu Saba wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri |
Mkazi wa Kijiji cha Mtanza, Yusufu Nyamgumi, akihoji kwenye mkutano kitendo cha Diwani wao, Athuman Mbange (CUF) kutokuwa na tabia ya kuwatembelea kujua matatizo yao, (PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269