Breaking News

Your Ad Spot

Sep 5, 2012

MKUTANO WA ASASI YA SIASA, ULINZI NA USALAMA NCHI ZA SADC (SADC TROIKA)

Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi ya Kusini mwa Afrika(SADC TROIKA) Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha siku moja cha asasi hiyo katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa SADC Rais Armando Emílio Guebuza wa Msumbiji na kati ni  Katibu Mtendaji wa SADC  Dkt Tomaz A. Salomao. Tukio hili linapatikana pia TANZANIA VISION BLOG Na kwa picha zaidi BOFYA HAPA 

1 comment:

  1. Ujumbe wangu kwa usalama wa ncho za Africa, ni kuwa na siasa za kikwetu za kupendana. Hebu angalia wenzetu huwezii kufika kwake kama hajakukaribisha, na ukimkuta anakula hawezi kukuambia karibu tule.
    Hii ni kuonyesha kuwa sisi tuna asili yetu, upendo na kujaliana ujirani. Sioni kwanini tupigane kwasababau ya mali asili. Sioni kwanini tuwe maadui kwasababu ya madaraka. Haya yote yaangalie kwa makini ni majaliwa ya muumba.
    Kaeni chini au wapeni majukumu haya wazee wenye hekima wajadili na kuweka mikakati ya kikwetu.
    Kwa mfano maziwa yanayounganisha nchi mbili, haya yawe ni sehemu ya kuungana, kila mmoj awe huru kutumia au nunu kwa nusu,...haya ya mali asili,...na haya yanaweza kujenga udugu wa kufanyiaan biashara. Sijui mimi nawaza nini, sioni kwanini ugombee kitu ambacho hujakitolea jasho!

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages