Breaking News

Your Ad Spot

Sep 28, 2012

NAPE: DK SLAA MWOGA WA KUSHINDWA

*Asema Dk. Slaa ameikimbia Mwanza mapema baada ya kunusa Chadema kugaragazwa
*Awapongeza madiwani wa CCM wa Nyamagana kwa kuwezesha ushindi wa Menya na Naibu Meya Nyamagana
NA MWANDISHI WETU, MWANZA
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema  dalili za kubwagwa kwa CHADEMA ndizo zilizomkimbiza mapema jijini Mwanza, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbroard Slaa.

Amesema kushindwa kwa Chadema katika kinyang’anyiro cha Meya na Naibu Meya, ni mavuno ya ubabe wa viongozi wa chama hicho ambao baadhi wanazeeka vibaya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Nape (pichani) alisema kwamba, Slaa alikimbia baada ya kuona maji yamezidi unga.

Nape aliyetumia fursa hiyo pia kuwapongeza Madiwani wa CCM wa wilaya ya Nyamagana na Chama kwa ushindi wa Viti vya Meya na Naibu wake, alisema Dk. Slaa anazeeka viba ndiyo maana naongoza chama hicho kwa ubabe na maandamano ya kila mara.

“Babu (akiwa na maana ya Dk Slaa) alisema CCM Mwanza itaondoka madarakani, imejidhihirisha wazi katika uchaguzi wa leo kuwa CCM bado ina nguvu na ni Chama kikongwe kisiasa, vingine vinaiga.”

“Chadema wameona mavuno ya ubabe wao japo kura za CCM ni ndogo…., Babu ajiulize kwa nini ameshindwa kwenye uchaguzi huo wa Meya na Naibu Meya.” Alisem Nape na kuongeza kwamba, kutokana na dalili za kushindwa zilizoonekana mapema, ndiyo maana Dk Slaa alikimbia Mwanza mapema.

Akiwapongeza madiwani hao kwa ushindi alisema kwamba wamefanya kazi kubwa na ya ziada kuhakikisha CCM inarejesha Halmashauri ya jiji hilo mikononi mwake baada ya kushikwa na Chadema kwa kipindi kifupi na hivyo kuwataka wana Mwanza wawe na mshikamano na kuwapa ushirikiano viuongozi wao.

“Nawasihi wananchi wa Mwanza wawe  na mshikamano na kuacha maandamano yasiyokuwa na msingi, badala yake wafanye maandeleo, waimamini CCM sasa inachokuja kufanya ni cha uhakika.” Alieleza Nape.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages