Breaking News

Your Ad Spot

Sep 14, 2012

POLISI WATATU WAFARIKI KATIKA AJALI YA GARI WAKATI WAKISAFIRISHA MAITI YA MWENZAO

SINGIDA, TANZANIA
Polisi watatu wa kike wamefariki dunia papo hapo baada ya gari walilokuwemo wakisafirisha maiti ya polisi mwenzao kupinduka leo asubuhi mkoani Singida.

Polisi waliofariki wametajwa kuwa ni SRosemary Nyabuzuki, Rehema Juma na Nyamwenda Juma

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, Linus Sinzumwa amesema kuwa polisi hao wakiwa na wanzao wanane walikuwa wakisafiri kwa gari la polisi  lenye namba PT 1149 wakitokea Morogoro mjini, wakisafirisha mwili wa polisi Regu Kamamo kwenda mkoani Mara.

Sinzumwa amesema ajali hiyo imetokea karibu na kambi ya Wachina, eneo la kijiji cha Manguanjuki, leo saa 5.30 asubuhi, kwa gari kupinduka kutokana na sababu ambayo haijajulikana.

Alisema majeruhi wanane  wa ajali hiyo wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida, na hali zao zinaendelea vizuri.


No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages