Breaking News

Your Ad Spot

Oct 14, 2012

AJALI YAUA WATANO BAHI


WATU watano wamekufa na wengine 14 kujeruhiwa, baada ya gari walimokuwa wakisafiria  kupinduka Wilaya ni Bahi mkoani hapa.

Ajali imehusisha  gari aina ya Toyota Hiece yenye namba za usajili T 803 ABX.

Akithibisha kutokea ajali hiyo,  Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa, alisema kwa simu kwamba, ilitokea leo saa 10.00 jioni eneo la Bahi Relini.

Betty alisema gari hiyo  ilikuwa ikiendeshwa na Yohana Samson, ikitokea Dodoma kwenda katika eneo la Makanda.

Alisema iliacha njia baada ya lori aina ya Scania lilokuwa likiendeshwa na Tutu Jackson kutaka kuipita kisha kurudi kwa ghafla barabarani na kisha kuligonga kwa nyuma Hiace hiyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages