Breaking News

Your Ad Spot

Oct 16, 2012

MSAFARA WA WAJUMBE KATIKA UCHAGUZI WA CCM MKOA WA MWANZA WAPATA AJALI, DEREFA AFARIKI PAPOHAPO


MWANZA, TANZANIA
Dereva amekufa na watu wengine 23, wakiwemo Wajumbe 20 wa Mkutano Mkuu wa CCM mkoani hapa kutoka wilayani Kwimba, Ofisa wa TAKUKURU, kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka wilayani humo, kupinduka.

Ajali hiyo ilitokea leo asubuhi, eneo la Buhongwa katika barabara kuu ya Mwanza-Shinyanga, wilayani Nyamagana, ambapo dereva wa basi hilo la Kampuni ya Bedui, alikufa papo hapo.

Basi hilo lenye namba za usajiri T. 853 BRB, linalofanya safari zake kutoka jijini Mwanza kwenda Mbarika wilayani Misungwi, lililokuwa limekodiwa na Chama kusafairisha wajumbe hao kutoka na kurudi wilayani Kwimba, liligongana na lori la Kampuni ya Nyanza Roads.

Kwa mujibu wa viongozi hao, Wajumbe 13 kati ya 20 waliopata ajali hiyo, walitibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando na kuruhusiwa kuondoka, lakini sita wakiwemo Madiwani wanne ambao hali zao zinadaiwa kuwa mbaya, wamelazwa.

Mwenyekiti wa CCM wilayani Kwimba, Peter Ng’hingi, ameuambia mtandao huu, kwamba, basi hilo lilikuwa na watu 23 wakiwemo Wajumbe wake na ofisa mmoja wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wa wilaya hiyo ambaye ni miongoni mwa watu waliolazwa kutokana na kuumia vibaya.

“Roli hilo tipper liliingia barabarani kwa ghafra na kusababisha Dereva wa basi letu aliyekufa papohapo, ashindwe ku control gari lake na hivyo kugonga ubavuni mwa roli na kupinduka.” Alisema Marando.

Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Lily Matola akizungumza kwa njia ya simu jana, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kwamba taarifa kamili zitatolewa na jeshi lake ambalo lilikuwa kwenye eneo la tukio, litatoa taarifa kamili baadaye.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages