Breaking News

Your Ad Spot

Oct 6, 2012

WATOTO U7 KUSAFIRI BURE KWENYE TRENI, LAKINI KWA MASHARTI


DAR ES SALAAM, TANZANIA
KAMPUNI  ya Reli Tanzania (TRL) limesema kuanzia sasa Watoto chini ya umri wa miaka saba, watasafiri bila malipo na watapewa viti yaani siyo kama katika daladala za jiji la Dar es Salaam, ambako ni dhambi mtoto kukaa kitini.

"Tunapenda kuwafahamisha wasafiri wetu wa Reli ya Kati wa daraja la tatu kwamba kuanzia sasa watoto chini ya miaka saba watasafiri bure na watapewa kiti/viti" limesema tangazo la TRL, lililotolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo A.Kisamfu na kuchapishwa leo kwenye baadhi ya vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa tangazo hilo watoto lazima wawe wamesafiri na wazazi au walezi wao lakini kasheshe kubwa ni kwamba lazima wawe na vyeti vya kuzaliwa au barua ya serikali za mtaa ya uthibitisho wa mhusika na mzazi au mlezi.

TRL inasema, vitambulisho hiyo lazima vionyeshwe wakati mzazi au mlezi anakata tiketi na msafiri anaruhusiwa kusafiri na watoto wawili tu kwa wakati mmoja na watoto watapewa tiketi maalum za watoto na kwamba mtoto atakayekutwa kwenye treni akiwa hayupo kwenye utaratibu, atalipishwa nusu nauli ya mtu mzima.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages