Luteni Kanali Mstaafu, Shimbo akiwa katika gari maalum leo |
DAR ES SALAAM, TANZANIA
MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamnyange amesema wataendelea kuutambua mchango wa Mnadhimu Mkuu Mstaafu wa jeshi hilo, Luteni Jerenali Abdulrahman Shimbo.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Mwamnyange wakati wa sherehe ya kumwuaga Mnadhimu huyo iliyofanyika katika kambi ya jeshi ya Mgulani jijini Dares Salaam. “Ni kiongozi ambaye ametoa mchango wake mkubwa tangu alipokuwa askari hadi Afisa wa ngazi za juu,” alisema Mwanyange.
Mwamnyange aliongeza kuwa Shimbo, ambaye ametumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 41 alikuwa ni mchakapazi wa hali ya juu, mwadilifu na mwenye nidhamu.
Akizungumzia kuhusu utendaji wake wa kazi, Shimbo alisema ni kitu cha kujivunia kwani nchi imeendelea kuwa na amani na usalama na kusema kwamba alijithidi kudumisha nidhamu na kuwafanya wanajeshi kuwa karibu na wananchi na kuwa wazalendo na upendo kwa nchi yao.
Shimbo alisema miongoni mwa changamoto ni kushindwa kutekeleza majukumu ya jeshi kutokana na uwezo mdogo wa kifedha.
Mnadhimu huyo aliagwa kwa gawaride na kusindikizwa na gari kutoka uwanja wa kambi hiyo hadi lango kuu ambalo lilisukumwa na maofisa wenye vyeo vya Meja Jenerali na baadaye Mwamnyange alimkabidhi funguo wa gari aina ya Landcruser ikiwa ni zawadi ya utumishi wake. Picha zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269