Breaking News

Your Ad Spot

Nov 7, 2012

MWENYEKITI WA CCM RAIS KIKWETE AKAGUA KIWANJA CHA MAKAO MAKUU YA CHAMA, UKARABATI WA KUMBI ZA MIKUTANO, DODOMA

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo juu ya ukarabati wa ukumbi wa mikutano wa 'White House' ulio katika makao makuu ya CCM mjini Dodoma ambao unafanyiwa ukarabati mkubwa ili kukidhi mahitaji ya sasa, Novemba 6, 2012.  Wanaompa maelezo ni Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama na Naibu Katibu Mkuu (Bara) John Chiligati. Nyuma yao ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa.

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongiozi wengine wakipata maelezo toka kwa Katibu Mkuu wa CCM Bw. Wilson Mukama juu ya maandalizi ya ujenzi wa makao makuu na vitega uchumi wa chama hicho mjini Dodoma ambako alisimama kwa muda siku ya Jumanne Novemba 6, 2012 akitoka katika ziara ya kikazi mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida alikokagua jumla ya miradi 19 ndani ya wiki moja.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua maandalizi ya ukumbi utaotumika wakati wa mkutano Mkuu wa CCM ulio kitongoji cha Kizota mjini Dodoma. Rais Kikwete alisimama kwa muda mjini Dodoma siku ya Jumanne Novemba 6, 2012
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua maandalizi ya ukumbi utaotumika wakati wa mkutano Mkuu wa CCM ulio kitongoji cha Kizota mjini Dodoma. Rais Kikwete alisimama kwa muda mjini Dodoma siku ya Jumanne Novemba 6, 2012
Mafundi rangi wakiwa kazini kuweka mambo sawa nje ukumbi utaotumika wakati wa mkutano Mkuu wa CCM uliopo,Kizota mjini Dodoma

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages