Breaking News

Your Ad Spot

Dec 4, 2012

JUMUIYA YA WATANZANIA LUTON - UINGEREZA NDUGU NA MARAFIKI WAMUAGA MARIAGORETH NDANGIO


Leo Tarehe 04/12/12 asubuhi muda wa saa tano watanzania waishio Luton Uingereza, Ndugu na marafiki kwa ujumla walijumuika kataka kanisa la Kikatoliki la Holy Ghost  Westbourne Luton Uingereza katika ibada ya kumuaga MariaGoreth (pichani) kabla ya kusafirishwa kurejea nyumbani kwao Tanzania kwa ajili ya mazishi.

Katika ibada hiyo mama mzazi wa marehemu aliwashukuru watu wote waliojitoa kwa kila hali wakati wa kumuuguza mwanae mpaka mauti ilipomkuta. Pia kaka wa marehemu alisoma historia fupi ya marehemu na  upendo na ushirikiano alikuwa nao na watu wote.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kesho Jumatano kuelekea Tanzania kwa ajili ya mazishi.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Luton ( Luton Tanzanian Community ) Bw. John Mbwete kwa niaba ya Familia ya marehemu na Jumuiya anatoa shukrani kubwa kwa watu wote waliojitoa kwa hali na mali, ubalozi wa Tanzania UK na Tanzania Association kwa ushirikiano waliotupa katika kufanikisha safari ya mwisho ya MARIAGORETH Kuelekea Tanzania.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa sifa na utukufu kwa Mwenyezi Mungu. 
                                                Shukrani 
                                    ABRAHAM SANGIWA
                        Katibu – Luton Tanzanian Community ( TLC )

1 comment:

  1. Hi tо all, thе cоntеnts exiѕting
    at this web pаge are really remarkаble for pеople knоwledge,
    well, κеep up the good work fellοws.
    Feel free to visit my blog youtu.be

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages