Breaking News

Your Ad Spot

Dec 31, 2012

RAIS KIKWETE AZINDUA MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI ILIYOFANYIKA TANZANIA MAPEMA MWAKA 2012

Hii ndiyo idadi ambayo imetangazwa na Rais Jakaya Kikwete leo kwenye uzinduzi matokeo ya Sensa iliyofanyika nchini kote mapema mwaka huu (2012)
 Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na wananchi wakati akisoma hotuba yake ya kutangaza rasmi uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi, leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Rais Jakaya, alisema kuwa katika Sensa ya mwaka huu, watanzania wameongezeka kwa asilimia kubwa ukilinganisha na Sensa iliyofanyika kwa mara ya kwanza nchini ya mwaka 1967, ambapo Watanzania wote walikuwa ni Milioni 12, 313, 054, na Tanzania Bara walikuwa ni milioni 11, 958,654 na Visiwani Zanzibar, walikuwa ni 354, 400, ambapo baada ya mwaka huo, Sensa kama hiyo ilifanyika tena mwaka 1978, 1988,2002 na hii ya mwaka huu 2012, ambapo imetoa idadi ya Watanzania wote kuwa ni jumla ya Milioni 44, 929,002. 
 Baadhi ya Madiwani na viongozi mbalimbali wa Serikali, waliohudhuria katika hafla hiyo leo.
 Kikundi cha Uhamasishaji cha Temeke, akikiwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kilichokuwa kikiendelea na kazi yake ya uhamasishaji uwanjani hapo.
 Sehemu ya wananchi waliojitokeza kuhudhuria hafla hiyo.
 Bendi ya THT, kutoka (kulia) ni Marlow, Amin na Linah, wakitoa burudani jukwaani wakati wa hafla hiyo.
 Wananchi wakisebeneka kushangilia baada ya Rais Jakaya Kikwete, kutangaza rasmi matokeo hayo ya Sensa.
 Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
 Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
 Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba, wakati akiondoka katika viwanja vya Mnazi Mmoja, baada ya kuzidua rasmi matokeo ya Sensa ya watu na makazi.

1 comment:

  1. HIZI TAARIFA ZA SENSA NI MUHIMU ZIANZE MARA MOJA KUTUMIKA KUWAPATIA HUDUMA SAHIHI WATANZANIA NI VEMA ZITUMIKE KIKAMILIFU KUANDAA BUDGET YA MWAKA 2013/2014 SI VEMA KUENDELEA KUCHAKACHUA UTOAJI WA HUDUMA NI VEMA WANANCHI WASHIRIKISHWE KIKAMILIFU KUTIMIZA WAJIBU WAO TUSIZOEE KUDAI HAKI TU

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages