Breaking News

Your Ad Spot

Dec 27, 2012

WATANO WAFARIKI DUNIA MOROGORO KATIKA MATUKIO TOFAUTI IKIWEMO AJALI YA GARI


MOROGORO. Tanzania
WATU watano wamefariki dunia mkoani Morogoro katika matukio tofauti, ikiwemo ya ajali ya gari ambayo ilisababisha kifo cha mmoja na kujeruhi wengine watano.

Aidha mwingine amekutwa kando kando mwa Reli ya TAZARA  akiwa amekufa huku mwili wake ukiwa na majeraha yanayodhaniwa alipigwa na kitu chenye ncha kali.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa Faustini Shilogile, alisema tukio la kwanza lilitokea Desemba 12, mwaka huu saa 10 jioni eneo la Luvili Mtimbila Wilaya ya Ulanga, Likihusisha gari kupata ajali na kusababisha kifo kwa Beatrice John (30) mkazi wa Ifakara Wilayani Kilombero.

Aliwataja waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo kuwa ni Gervas Salamba (49) mkazi wa Dar es salaam,  Sabrina Mlongile (45), Chrisi Kalvin (29) wakazi wa  Ifakara Wilayani Kilombero na  Tetemula Madirisha (32), Sahan Madirisha wakazi wa  Malinyi Wilayani Ulanga, 

Kamanda, alisema majeruhi wote walitibiwa katika hospitali ya Lugala na kuruhusiwa,  huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo, ambapo chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa gari hilo.

Alilitaja gari hilo  kuwa ni lenya namba za usajiri T 709 BTN aina ya Toyota Noah iliyokuwa ikiendeshwa na Hassan Popo (49) mkazi wa Ifakara ikitokea  Mtimbila kuelekea Ifakara , na kwamba  dereva huyo,a nashikiliwa atafikishwa mahakamani  mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Katika tukio la pili Mwanaume mmoja, Matei Kitinde (45) mkazi wa  kijiji cha Mambogi  alikutwa amefariki hatua 50 kutoka katika reli ya TAZARA huku mwili wake ukiwa na majeraha kichwani, ubavuni na mkono wa kulia  yanayoonesha kuwa alipigwa na kitu chenye ncha kali.

Alisema tukio hilo lilitokea Desemba 26 mwaka huu sa 2:30 asubuhi katika eneo la Kiberege Tarafa ya Mang’ula Wilayani Kilombero na kwamba hakuna mtu yeyeote aliyekamatwa kuhusika na mauaji hayo na polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini waliohusika.

Akizungumzia tukio la tatu alisema Mfanyakazi wa Mashamba ya Miwa ya umwagiliaji katika Kiwanda cha Sukari Kilombero (ILLOVO) Gemson Kaduma (45) mkazi wa Kijiji cha Msokwa aliktwa amefariki kwenye mashamba hayo Desemba 12 huku akiwa amelalaliwa na mambomba ya kumwagilia miwa nakwamba uchunguzin unaendelea.

Katika tukio la nne mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Masanja (37) mkazi wa Ilonga Wilayani Kilosa amekutwa amefariki baada ya kuuwawa na watu wasiojulikana katika eneo la mashamba ya Mbegu ya Msimba Wilayani humo .

Alisema tukio hilo lilitokea Desemba 24 mwaka huu saa 5 asubuhi katika mashamba hayo, ambapo mikono ya marehemu huyo ilikutwa imefungwa kwa nyuma na kamba ya katani huku sababu za kifo hicho zikielezwa  kuwa zilitokana na kipigo kikali, na kwamba uchunguzi unaendelea kubaini waliohusika na mauaji hayo.

Katika tukio la tano alisema lilitokea Desemba 24 saa 1:30 usiku katika eneo la Morogoro Hotel Manispaa ya Morogoro ambapo  mtembea kwa miguu asiyefahamika mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 45 hadi 55 alifariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na pikipiki.

Hata hivyo alisema mwili wa mwanaume huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa wa Morogoro,nakwamba aligongwa na pikipiki isiyofahamika namba iliyokuwa ikiendeshwa na Eliyopo Devid ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na  mkazi wa Foresti  Mjini hapa.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages