Breaking News

Your Ad Spot

Feb 26, 2013

MeTL GROUP YAPATA TUZO


Mkurugenzi kutoka taasisi ya Superbrands ukanda wa Afrika Mashariki, Jawad Jaffer akitoa maelezo kwa wageni waalikwa juu ya kitabu cha orodha ya kampuni zilizotunukiwa hadhi ya Superbrands wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti vya tuzo za ubora na thamani ya nembo kwa makampuni bora 2013/14 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa taasisi huru ya Superbrands Ukanda wa Afrika Mashariki Jawad Jaffer akimkabidhi Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji cheti cha tuzo ya ubora na thamani ya nembo kwa kampuni zinazotoa huduma bora kwa walaji katika hafla fupi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Raha Aashiq Sharrif (Kulia) akiwa Mwakilishi wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Raha Preetkamal Bansal ( wa pili kulia) wakati wa hafla fupi ya Superbrands kukabidhi vyeti kwa makampuni bora kwa mwaka 2013/14 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa ITV na Radio One Bi. Joyce Mhaville ( wa pili kulia) aliyembatana na Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha IPP Bi. Joyce Luhanga ( wa tatu kulia) wakati wa hafla ya utoaji wa cheti cha tuzo ya ubora na thamani ya nembo iliyoendeshwa na Taasisi ya Superbrands.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji akibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa katika hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages