Breaking News

Your Ad Spot

Feb 11, 2013

UCHAGUZI WA KAMATI KUU YA CCM WAFANYIKA JIONI HII

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akipiga kura yake katika uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, uliofanywa na Wajumbe wa NEC, leo kwenye ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Wengine kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
 Makatibu wa NEC, Zakia Meghji (Uchumi na Fedha) na Dk. Asha-Rose Migiro (Siasa na Uhusiano wa Kimataifa) wakipiga kura,  wakati wa uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM uliofanywa na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, jioni hii, wakati wa Kikao cha NEC kilichofanyika katika ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
 Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Wilson Mukama akipiga kura  wakati wa uchaguzi huo
Kikwete akizungumza na wajumbe wa NEC, wakati wakisubiri matokeo baada ya uchaguzi hu. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages