Breaking News

Your Ad Spot

Feb 13, 2013

UNAFIKIRI NINI KITATOKEA KAMA MTUME MUHAMMAD (SAW) NA YESU KRISTU WATAKUTANA LIVE?



Nchini Tanzania dini kubwa ni Ukristo na Uislamu. Kila dini hufundisha wafuasi wake kuamini kwamba dini husika ndiyo sahihi na pekee itakayoweza kumfikisha mtu katika uzima wa milele au peponi. Je, ulishawahi kujiuliza kama itatokea nini Yesu Kristo a.k.a mwana wa Mungu akikutana live na Mtume wa Mungu a.k.a Allah, Muhammad (S.W.A) mitaa fulani ya Kkoo, ubungo au hata Manzese?  Watatwangana ngumi au kurushiana matusi kama vile fala, Mshenzi, pagani, kafri nk?

Kama unafikiri hivyo umepotea sana ndugu. Haya magwiji yakikutana yatacheeeeka sana, yatakumbatiana na kuwa na stori kibao za kazi wanayoifanya ya kukomboa roho zenu! watashangaa sana kuona wajinga mnabishana, kutukanana, kupigana na hata kuuana kisa wao! watawakemea vibaya sana na kuwaonya mwache uchizi ndugu! Hizo ndizo salam zandu kwenu wadau wa Mtandao huu. Kama kuna anayewaza tofauti anijulishe hapa hapa auwaemailhii:- jlkamala@gmail.com,  WENU Kamala J Lutatinisibwa

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages